An-Nahl
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَمِن ثَمَرَٰتِ ٱلنَّخِيلِ وَٱلْأَعْنَـٰبِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا حَسَنًا ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ 67
{67} Yeye Mtukufu alifanya matunda ya mitende na zabibu kuwa na manufaa na masilahi kwa waja wake kama vile aina mbalimbali za riziki nzuri ambayo waja wake hula ikiwa laini na imeiva, iliyopo na iliyowekwa kama akiba, na kama chakula na kinywaji kinachotengenezwa kutoka kwa juisi yake na maji matamu ya matunda, na mvinyo ambao ulikuwa halali kabla ya hapo. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaharamisha vileo na akaweka badala yake vilivyo vizuri miongoni mwa maji matamu ya matunda na aina mbalimbali za vinywaji vitamu ambavyo vinaruhusiwa. Basi ndiyo maana wakasema baadhi yao kilichokusudiwa na 'Sakar' hapa ni chakula na kinywaji kitamu, na kauli hii ndiyo inayofailia zaidi kuliko kauli nyingine ile. "Hakika katika hayo ipo Ishara kwa kaumu watumiao akili," katika maneno ya Mwenyezi Mungu kwamba yeye ni mkamilifu wa uwezo, ambapo alivitoa kutoka katika miti inayofanana na kuni, kisha zikawa mazao yenye ladha na matunda mazuri. Na pia wanazingatia ujumla wa rehema yake, ambapo aliwaenea waja wake wote kwa hayo na akawafanyia kuwa mepesi. Na pia wanazingatia kwamba yeye ndiye Mungu aabudiwaye peke yake, kwa maana Yeye ni wa pekee katika hayo.