U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ibrahim
Suuradda 14

Ibrahim

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 13

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِرُسُلِهِمْ لَنُخْرِجَنَّكُم مِّنْ أَرْضِنَآ أَوْ لَتَعُودُنَّ فِى مِلَّتِنَا ۖ فَأَوْحَىٰٓ إِلَيْهِمْ رَبُّهُمْ لَنُهْلِكَنَّ ٱلظَّـٰلِمِينَ 13

{13} Alipotaja ulinganiaji wa Mitume kwa kaumu zao na kudumu kwao katika hilo bila ya kuchoka, akataja hali ya mwisho zaidi waliyofika na kaumu yao, akasema: "Na wale waliokufuru wakawaambia Mitume wao" huku wakiwatishia, "Hakika tutawatoa katika nchi yetu, au lazima mrudi katika mila yetu" Na hili ndilo jibu kubwa zaidi, ambalo baada ya hili hakuna matumaini yoyote juu yao. Kwa sababu haikutosha tu kuupa mgongo uwongofu, bali waliwatishia kuwatoa katika makazi yao, na wakayaita makazi hayo kwamba ni yao, na wakadai kuwa Mitume hawana haki yoyote humo. Na hii ndiyo dhuluma kubwa kabisa. Kwani Mwenyezi Mungu aliwatoa waja wake wakaja kwenye ardhi, na akawaamrisha kwamba wamwabudu, na akaitiisha ardhi na vyote vilivyomo kwa ajili yao, ili watafute msaada wa hayo katika kumwabudu. Kwa hivyo, Yeyote anayetumia hayo kumsaidia kumwabudu Mwenyezi Mungu, basi ni hivyo vinakuwa halali kwake na hawi wa kulaumiwa. Na mwenye kutafua msaada wa hivyo katika kukufuru na aina mbalimbali za madhambi, hivyo haviwezi kuwa vyake tu wala haviwi halali kwake. Kwa hivyo akajulikana kwamba maadui wa Mitume kwa hakika hawakuwa na chochote katika ardhi ambayo waliwatishia Mitume kwamba watawatoa humo. Na hata kama tutarudi katika desturi, Mitume ni miongoni mwa wakazi wa nchi zao na watu miongoni mwao. Basi ni kwa kitu gani wanawazuia kuwa na haki ya moja kwa moja na iliyo wazi? Je, haya si chochote isipokuwa ukosefu kamili wa dini na uungwana? Na ndiyo maana njama zao dhidi ya Mitume zilipoishia katika hali hii, haikubakia isipokuwa Mwenyezi Mungu kupitisha amri yake na kuwanusuru marafiki wake. "Basi Mola wao Mlezi aliwafunulia wahyi: Hakika tutawaangamiza madhalimu" kwa aina mbalimbali za adhabu.