Hud
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَلَقَدْ جَآءَتْ رُسُلُنَآ إِبْرَٰهِيمَ بِٱلْبُشْرَىٰ قَالُوا۟ سَلَـٰمًا ۖ قَالَ سَلَـٰمٌ ۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجْلٍ حَنِيذٍ 69
{69} Yaani, "Na hakika wajumbe wetu walimjia;" yaani, wajumbe hao walikuwa Malaika watukufu, nao walimjia Mtume wetu "Ibrahim" Al-Khalil "kwa bishara njema." Yaani, kwa habari njema ya kupata mtoto wakati Mwenyezi Mungu alipowatuma kuwaangamiza kaumu ya Lut na akawaamuru kwamba wapitie kwa Ibrahimu na wampe bishara njema ya kuzaliwa kwa Is-haq. Basi walipoingia kwake, "wakasema, "Salama!" Naye akasema, "Salama!" Yaani, walimsalimia naye akawajibu salamu zao. Na katika hili kuna uhalali wa kutoa salamu, na kwamba haikuacha kuwa katika mila ya Ibrahim, amani iwe juu yake, na kwamba salamu huwa kabla ya mazungumzo, na kwamba inafaa jibu liwe bora zaidi kuliko kuanzisha salamu. Kwa sababu katika maamkizi yao walitumia sentensi ianzayo kwa kitenzi, kitu ambacho kinaonyesha upya, naye akajibu kwa sentensi ianzayo kwa nomino jambo linaloonyesha uthabiti na uendelevu, na kuna tofauti kubwa kati ya mawili hayo, kama inavyojulikana katika sayansi za lunga ya Kiarabu. "Kisha hakukaa" Ibrahimu walipoingia kwake "mara hiyo akaja na ndama wa kuchoma." Yaani, alikwenda haraka nyumbani na akawaletea wageni wake ndama wa kuchomewa kwenye mawe ya moto, mnene; basi akamsongesha karibu nao na akasema: Mbona hamli?