U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · Hud
Suuradda 11

Hud

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 35

أَمْ يَقُولُونَ ٱفْتَرَىٰهُ ۖ قُلْ إِنِ ٱفْتَرَيْتُهُۥ فَعَلَىَّ إِجْرَامِى وَأَنَا۠ بَرِىٓءٌ مِّمَّا تُجْرِمُونَ 35

{35} "Au ndio wanasema: Ameizua?" Kiwakilishi nafsi hiki 'a' kinaweza kumrudia Nuhu, kama ulivyokuwa muktadha katika hadithi yake na kaumu yake, na kwamba maana yake ni: hakika kaumu yake wanasema: Amemzulia uongo Mwenyezi Mungu, na akaudanganyishia wahyi ambao anadai kuwa umetoka kwa Mwenyezi Mungu. Na kwamba Mwenyezi Mungu alimuamrisha kwamba aseme: "Sema: Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu, na mimi niko mbali sana na makosa myatendayo." Yaani, kila mmoja atabeba mzigo wake, "Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine." Na inawezekana kwamba inamrudia Nabii Muhammad -rehema na amani ziwe juu yake - na aya hii imeingilia tu kati kwenye kisa cha Nuhu na kaumu yake. Kwa sababu, ni miongoni mwa mambo ambayo hawayajui isipokuwa manabii peke yao. Basi Mwenyezi Mungu alipoanza kumsimulia Mtume wake juu yake, na yakawa miongoni mwa ishara zinazoashiria ukweli wake na ujumbe wake, Akataja kukanushwa kwake na kaumu yake kwa maelezo kamili, na akasema: "Au ndio wanasema: Ameizua?" Yaani, Qur-ani hii aliizua Muhammad mwenyewe tu. Basi haya ni katika kauli za kushangaza batili zaidi na zilizo batili zaidi. Kwani, Wanajua kwamba yeye hakusoma, wala hakuandika, wala hakusafiri akawaacha akaenda kusoma kwa watu wa vitabu; basi ndiyo akaleta kitabu hiki ambacho kiliwapa changamoto ya kuleta sura moja mfano wake. Kwa hivyo, wakidai pamoja na haya kuwa yeye ndiye aliyeizua, basi itajulikana kuwa wao ni wakaidi tu, na hakutakuwa na faida yoyote katika kuhojiana nao. Bali katika hali hii, kinachofailiana nao zaidi ni kujitenga nao, na kwa sababu ya hili ndiyo akasema: "Sema, "Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu." Yaani, dhambi yangu na uongo wangu. "Na mimi niko mbali sana na makosa myatendayo." Yaani, kwa nini mnang'ang'ania kunikadhibisha.