Yunus
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَمَا تَكُونُ فِى شَأْنٍ وَمَا تَتْلُوا۟ مِنْهُ مِن قُرْءَانٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚ وَمَا يَعْزُبُ عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا فِى ٱلسَّمَآءِ وَلَآ أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكْبَرَ إِلَّا فِى كِتَـٰبٍ مُّبِينٍ 61
{61} Yeye Mtukufu anajulisha juu ya ujumla wa kuona kwake na kujua kwake hali zote za waja wake katika harakati zao na utulivu wao. Na ndani ya hili kuna wito wa kumchunga Yeye daima, akasema: "Na huwi katika jambo lolote." Yaani, hali yoyote miongoni mwa hali zako za kidini na za kidunia, "wala husomi sehemu yoyote katika Qur-ani." Yaani, na chochote unachokisoma katika Qur’ani ambayo Mwenyezi Mungu alikufunulia, "wala hamtendi kitendo chochote" kidogo au kikubwa, "isipokuwa Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo." Yaani, wakati mnapoyaanza, na kuendelea kuyafanya. Basi mchungeni Mwenyezi Mungu katika vitendo vyenu, na vifanyeni kwa njia ya uaminifu na kujitahidi. Na jihadharini na yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani, Yeye anawaona na anajua dhahiri zenu na ndani zenu. "Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi;" yaani, hakifichiki juu ya kujua kwake, na kusikia kwake, na kuona kwake, na kushuhudia kwake "chenye uzito hata wa chembe katika ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa isipokuwa kimo katika Kitabu kilicho wazi." Yaani, amekwisha kizunguka kwa elimu yake, na kalamu yake ikayaandika. Na daraja mbili hizi katika daraja za hatima na mapitisho mara nyingi Mwenyezi Mungu huziunganisha pamoja, ambazo ni elimu inayozunguka vitu vyote, na kuandika kwake kunakozunguka matukio yote, kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Je, hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yako katika Kitabu. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi."