Yunus
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ 48 قُل لَّآ أَمْلِكُ لِنَفْسِى ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ ۗ لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۚ إِذَا جَآءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَـْٔخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ 49
{48 - 49} Basi na watahadhari wale wanaokukadhibisha kujifananisha na umma walioangamizwa, kwa hivyo yakawapata yale yaliyowapata watu wale, wala wasione kwamba adhabu itachelewa na wakasema, "Ni lini ahadi hii, ikiwa nyinyi ni wakweli?" Kwani huu ni udhalimu kutoka kwao, kwa sababu walitaka hilo kutoka kwa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. – Yeye hakika hana chochote katika jambo hili, bali juu yake ni kufikisha tu na kuwabainishia watu. Na ama hesabu yao na kuteremsha adhabu juu yao, basi hilo ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mtukufu. Ataiteremsha juu yao utakapofika muda ambao aliliwekea hilo na wakati ambao alipitisha lifanyike ndani yake ambao unaafikiana na hekima Yake ya kiungu. Basi wakati huo unapokuja, hawawezi kukawia hata saa moja wala hawawezi kutangulia. Basi na watahadhari wanaokadhibisha kuiharakisha. Kwa maana wanaiharakisha adhabu ya Mwenyezi Mungu ambayo inapoteremka, basi adhabu yake haizuiliki dhidi ya kaumu wahalifu. Na kwa sababu hii akasema: