Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Surah 9

At-Tawba

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 72

وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا وَمَسَـٰكِنَ طَيِّبَةً فِى جَنَّـٰتِ عَدْنٍ ۚ وَرِضْوَٰنٌ مِّنَ ٱللَّهِ أَكْبَرُ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ 72

{72} Kisha akataja yale aliyoandaa Mwenyezi Mungu kwa ajili yao miongoni mwa malipo, kwa hivyo akasema: {Mwenyezi Mungu amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Bustani zipitiazo mito chini yake" zinazokusanya neema zote na furaha, zisizokuwa na udhia wowote na huzuni, inapita chini ya kasri zake, na majumba yake na miti yake mito mingi inayomwagilia mabustani mazuri ambayo hajui yale yaliyo ndani yake ya heri nyingi, baraka tele isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. "Watadumu humo." Hawatatafuta kutoka humo. "Na makazi mema katika Bustani za kudumu" ambazo tayari zilipambwa, na kurembeshwa, na kutayarishwa kwa ajili ya waja wa Mwenyezi Mungu wachamungu. Tayari kunapendeza kuzitazama, na yanapendeza makazi yake na mahali pake na kupumzikia, na zimekusanya katika ala za makazi ya juu ambazo wenye kutamani hawawezi kutamani zipotee, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu amewaandalia vyumba vya hali ya juu zaidi na vizuri zaidi, ambavyo nje yake inaweza kuonekana kutoka kwa ndani yake, na ndani yake kutoka kwa nje yake. Basi haya ni makazi mazuri ambamo yanastahili zaidi kwamba nafsi zikae humo kwa utulivu, na ivutiwe kwayo mioyo, na roho zinayatamani sana. Kwa sababu ziko "katika Bustani za kudumu;" yaani, pa kukaa, hawataondoka humo wala kuhama kutoka humo. "Na Radhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu" anazofikishia watu wa Peponi "ndizo kubwa zaidi" kuliko neema walizo ndani yake. Kwani neema yao hiyo haikuwa nzuri kwao isipokuwa kwa kumuona Mola wao Mlezi na radhi zake juu yao, na kwa sababu ndilo lengo waliloliendea wenye kufanya ibada, na mwisho ambao waliwania kuufikia wale wanaompenda. Kwa hivyo ridha ya Mola Mlezi wa ardhi na mbingu zote ndiyo kubwa zaidi kuliko neema ya mabustani. "Huko ndiko kufuzu kukubwa" ambapo walipata kila kitafutwacho, na kikawaondokea kila kinachoepukwa, na mambo yote yakawawia mazuri na yenye kupendeza. Basi tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie miongoni mwao kwa ukarimu wake mkubwa.