At-Tawba
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
لَا يَزَالُ بُنْيَـٰنُهُمُ ٱلَّذِى بَنَوْا۟ رِيبَةً فِى قُلُوبِهِمْ إِلَّآ أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ 110
{110} "Na jengo lao hilo walilolijenga halitaacha kuwa shaka katika nyoyo zao” yaani shaka na kusitasita kuliobakia ndani ya nyoyo zao "mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande” kwamba wajute majuto makubwa, na watubie kwa Mola wao Mlezi, na wanamhofu hofu kubwa mno. Na kwa hayo Mwenyezi Mungu atawasamehe, vinginevyo, basi mjengo wao huo hauwaongezi isipokuwa shaka juu ya shaka yao, na unafiki juu ya unafiki wao. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema” mambo yote, ya dhahiri yake na ya nje yake, yaliyofichika yake, na yaliyo wazi yake, na yale waliyoyafanya waja kwa siri na yale waliyoyafanya wazi wazi. "Mwenye hekima;" hatendi, wala haumbi, wala haamrishi, wala hakatazi, isipokuwa kile kinachohitajiwa na hekima yake na akakiamrisha. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Na katika aya hizi kuna manufaa kadhaa. Miongoni mwake ni kujifanyia msikiti kwa makusudio ya kuudhuru msikiti mwingine ulio karibu nao ni haramu, na kwamba ni lazima kuubomoa msikiti huo wa madhara ambao makusudio ya wenyewe yamejulikana. Na miongoni mwake ni kwamba, kitendo hata kama ni kizuri zaidi, kinabadilishwa na nia, kwa hivyo kinageuka kuwa kulichokatazwa, kama nia ya wamiliki wa msikiti wa madhara ilivyobadilisha kitendo chao kikawa kama unavyoona. Na miongoni mwake ni kwamba, kila hali ambayo kwayo unatokea mgawanyiko baina ya waumini, basi hiyo ni katika maasia ambayo ni lazima kuyaacha na kuyaondoa, kama vile pia kila hali ambayo kwayo kunapatikana kujumuika na kuungana kwa waumini, basi ni lazima ifuatwe, na iamrishwe, ihimizwe juu yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alitoa sababu ya kujitengenezea kwao msikiti wa madhara kwa lengo hili ambalo linalazimu kuukataza kama linavyolazimu hilo ukafiri na kupigana vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na miongoni mwake ni kuharamishwa kuswalia katika sehemu za maasia na kukaa mbali nazo na pia katazo la kuzikaribia. Na miongoni mwake ni kwamba uasi unaathiri katika sehemu kama vile uasi wa wanafiki ulivyouathiri msikiti wa madhara na ikakatazwa kusimama ndani yake. Na vile vile utiifu unaathiri katika sehemu kama ulivyouathiri katika msikiti wa Quba, mpaka Mwenyezi Mungu Akasema juu yake: "Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa uchamungu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake.” Na kwa sababu ya hili, Msikiti wa Quba ukawa na ubora usiokuwa katika msikiti mwingineo kiasi kwamba yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – alikuwa akitembelea Quba kila Jumamosi akiswalia humo, na akahimiza juu ya kuswalia humo. Na miongoni mwake ni kwamba, tunaweza kujifunza Kanuni nne muhimu kutoka katika sababu zilizotajwa katika Aya hii, nazo ni: kila tendo lenye madhara kwa Muislamu, au lina maasia kwa Mwenyezi Mungu ndani yake, basi maasia ni katika matawi ya ukafiri, au ndani yake kuna kuwagawanyisha Waumini, au ndani yake kuna kuwasaidia wale wanaopigana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hilo limeharamishwa na limekatazwa. Na kinyume chake ni kama kinyume chake. [Na miongoni mwake ni kwamba, matendo ya kihisia yanayotokana na kutomtii Mwenyezi Mungu, hayaachi kuendelea kumweka mtendaji wake mbali na Mwenyezi Mungu ni sawa na kusisitiza kuendelea kuasi mpaka ayaondoe na atubie toba kamili kutokana nayo, kiasi kwamba moyo wake ukatike kwa majuto tena majuto makubwa.] Na miongoni mwake ni kwamba, ikiwa msikiti wa Quba uliasisiwa juu ya uchamungu, basi Msikiti wa Nabii – Rehema na Amani zimshukie – ambao aliouasisi kwa mkono wake uliobarikiwa, na akatenda humo matendo mema, na Mwenyezi Mungu akamchagulia mahali hapo basi unastahili zaidi na unafaa zaidi. Na miongoni mwake ni kwamba, tendo lililojengwa juu ya ikhlasi na kumfuata Mtume ndilo tendo lililojengwa juu ya uchamungu, lenye kumfikisha mtendaji wake kwenye mabustani ya neema. Nalo tendo lililojengwa juu ya nia mbaya, uzushi, na upotofu, basi hilo ni tendo lililoasisiwa juu ya ukingo wa shimo unaoporomoka, basi ukaporomoka naye ndani ya Moto wa Jahannam. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.