At-Tawba
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
أَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ هُوَ يَقْبَلُ ٱلتَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِۦ وَيَأْخُذُ ٱلصَّدَقَـٰتِ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ 104
{104} Yaani: Je, hawakujua upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu na ujumla wa ukarimu Wake, na kwamba Yeye "anakubali toba ya waja wake” wanaotubu kutokana na dhambi yoyote ile? Bali anafurahi Yeye Mtukufu kwa toba ya mja wake anapotubia, furaha kubwa kabisa anayoweza kukadiriwa, "na anazichukua sadaka” kutoka kwao. Yaani, anazikubali na anazichukua kwa kulia kwake, kisha anazikuza kwa ajili ya mmoja wao kama vile mtu anavyomkuza mwana farasi wake, mpaka tende moja inakuwa kama mlima mkubwa. Basi kitakuaje kilicho kikubwa zaidi na kingi zaidi ya hiyo? "Na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu sana?” Yaani, Mwingi wa kukubali toba kwa wale wanaotubu. Kwa hivyo, mwenye kutubia kwake, anamkubalia toba, hata kama maasia yake yatajirudia mara nyingi, na Mwenyezi Mungu hachoki kukubali toba ya waja wake mpaka wao wachoke, na wakatae isipokuwa kukimbia, na kuwa mbali na mlango wake, na kufanya urafiki wendani na adui yao. “Mwenye kurehemu sana” ambaye Rehema yake imekienea kila kitu, na ameiandikia wale wanaomcha, na wakatoa Zaka, na wanaziamini Ishara zake, na wanamfuata Mtume wake.