Al-Fajr
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
فَأَمَّا ٱلْإِنسَـٰنُ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكْرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَكْرَمَنِ 15 وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَهَـٰنَنِ 16 كَلَّا ۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ ٱلْيَتِيمَ 17 وَلَا تَحَـٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ 18 وَتَأْكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا 19 وَتُحِبُّونَ ٱلْمَالَ حُبًّا جَمًّا 20
{15 - 20} Mwenyezi Mungu anatuambia kuhusu asili ya mwanadamu jinsi alivyo, na kwamba yeye ni mjinga na dhalimu na hana elimu ya matokeo ya mambo. Anadhani kwamba hali inayompata itaendelea na haitaondoka, na anadhani kuwa kumtukuza ambako Mwenyezi Mungu anamtukuza katika dunia na neema zake anazompa vinaashiria heshima yake [kwake] na ukaribu wake kwake, na kwamba ikiwa "atampunguzia riziki yake" ikawa kiasi cha chakula kisichozidi mahitaji yake, kwamba hilo ni kumdunisha kutokako kwa Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu akamjibu dhana yake hii, akasema: "Sivyo hivyo!" Yaani, siyo kila niliyembariki katika dunia hii ni mtukufu kwangu, wala kila mtu ambaye nimempunguzia riziki yake ni duni mbele yangu. Bali utajiri na umasikini, wingi na dhiki ni majaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu na mtihani ambao kwa huo huwajaribu waja wake; ili kumuona anayemshukuru na kuwa na subira, ndiyo amlipe malipo makubwa kwa hayo. Na yule asiyekuwa hivyo, basi amhamishe hadi kwenye adhabu kali. Na pia; hima ya mja kusimamia tu kwenye kile anachokitaka tu ni katika hima dhaifu, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akawalaumu kwa kukosa kwao kujali masilahi ya wahitaji, kwa hivyo akasema: “Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima" aliyefiwa na baba yake na yule aliyekuwa akimchumia, na akahitaji wa kumliwaza na kumfanyia wema. Nyinyi hamumkirimu, lakini badala yake mnamtweza, na hili linaashiria ukosefu wa huruma katika nyoyo zenu na kutotaka kwenu mema. "Wala hamhimizani kulisha masikini" Na hili ni kwa sababu ya ubahili wenu juu ya mambo ya dunia na kuipenda sana ambako kumeimarika katika nyoyo zenu. Ndiyo maana akasema: "Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa" bila kubakisha kitu katika huo. "Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi." Na hili ni kama kauli yake: "Lakini nyinyi mnahiari maisha ya dunia! Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi." Na akasema "Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani. Na mnaacha maisha ya Akhera."