Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Muddaththir
Surah 74

Al-Muddaththir

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 31

وَمَا جَعَلْنَآ أَصْحَـٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَـٰٓئِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِيَسْتَيْقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ وَيَزْدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِيمَـٰنًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَٱلْكَـٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِىَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ 31

{31} "Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika" kwa sababu ya ukali wao na nguvu zao. "Wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha waliokufuru." Inawezekana kwamba kinachokusudiwa hapa ni 'isipokuwa kwa ajili wawaadhibu huko Akhera humo motoni na kuwazidishia humo adhabu. Adhabu pia inaitwa fitna (majaribio); kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Hiyo ni siku watakayoadhibiwa Motoni." Inawezekana kuwa kinachomaanishwa hapa ni kwamba hatukukuambieni juu ya idadi yao isipokuwa ili tujue ni nani anayesadiki na ni nani anayekadhibisha. Haya yanaonyeshwa na yale aliyoyataja baada yake katika kauli yake: "wapate kuwa na yakini wale waliopewa Kitabu, na wazidi Imani wale walioamini." Kwa maana, Watu wa Kitabu ikiwa haya yataafikiana na yale waliyo nayo na yakalingana, yakini yao juu ya haki inaongezeka. Nao Waumini kila Mwenyezi Mungu anapoteremsha Aya, wakaiamini na kuisadiki, imani yao inaongezeka. "Wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu na Waumini." Yaani, ili hilo liwaondoshee shaka na kusitasita. Na haya ni malengo makubwa wanayoyachunga mno wenye akili, ambayo ni kujitahidi kuwa na yakini na kuzidisha imani kila wakati na katika kila suala la dini, na kuondosha shaka na fikira potofu zinazojitokeza katika kukabiliana na haki. Basi akayafanya yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake kuwa ni yenye kufanikisha malengo haya makubwa, na yenye kupambanua wakweli mbali na waongo, na ndiyo maana akasema: "Na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao." Yaani, maradhi ya shaka, dhana na unafiki "na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu?" Haya ni katika njia ya kuchanganyikiwa na shaka kwa upande wao na kukufuru ishara za Mwenyezi Mungu. Na hili na lile ni sehemu katika kuongoa kwa Mwenyezi Mungu yule ambaye amemuongoa na upotoshaji wake kwa yule ambaye anampoteza, na ndiyo maana akasema: "Ndiyo kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye." Kwa hivyo yule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, anayafanya yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake kuwa ni rehema kwake na kuzidisha imani yake na dini yake, Na yule ambaye amempotosha, anayafanya yale aliyoyateremsha kwa Mtume wake kuwa ni kuzidisha upotofu juu yake, mkanganyiko na giza kwa upande wake. "Na hapana yeyote anayejua majeshi ya Mola wako Mlezi" miongoni mwa Malaika na wengineo "ila Yeye tu." Basi ikiwa nyinyi hamjui majeshi yake, na amekujulisheni hayo Mjuzi mno, Mwenye habari zote, basi lazima muamini habari zake bila ya shaka yoyote wala kusitasita. "Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binadamu." Wala hayakukusudiwa mawaidha haya na ukumbusho kuwa ni upumbavu na mchezo. Bali kilichokusudiwa kwayo ni watu kukumbuka yale yanayowanufaisha, wakayafanya, na yale yanayowadhuru, basi wakayaacha.