Al-An'aam
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
قُلْ أَىُّ شَىْءٍ أَكْبَرُ شَهَـٰدَةً ۖ قُلِ ٱللَّهُ ۖ شَهِيدٌۢ بَيْنِى وَبَيْنَكُمْ ۚ وَأُوحِىَ إِلَىَّ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانُ لِأُنذِرَكُم بِهِۦ وَمَنۢ بَلَغَ ۚ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ ٱللَّهِ ءَالِهَةً أُخْرَىٰ ۚ قُل لَّآ أَشْهَدُ ۚ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ وَإِنَّنِى بَرِىٓءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ 19
{19} "Sema," uwaambie tunapowabainishia uwongofu na tukawawekea wazi njia; "Ni kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa kabisa?" Juu ya kanuni hii kuu "Sema: Mwenyezi Mungu," ndiye shahidi mkubwa zaidi. Yeye ndiye "shahidi baina yangu na nyinyi;" kwa hivyo hakuna aliye mkuu zaidi yake wala mkubwa zaidi yake katika ushahidi. Naye ananishuhudia mimi kwa kukiri kwake na kitendo chake. Hivyo basi ananikiria kwa niliyowaambia, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno, basi bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo!" Basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye hekima, Mwenye uwezo, na wala haifai kwa hekima yake na uwezo wake kumkiria mwenye kumzulia uongo, akidai kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyemtuma na ilhali hakumtuma. Na kwamba, Mwenyezi Mungu alimwamrisha kuwalingania viumbe ilhali hakumwamrisha, na kwamba Mwenyezi Mungu alimruhusu kumwaga damu ya wale wanaomhalifu, na mali zao, na wanawake wao, naye pamoja na hayo anamsadiki kwa kumkiria kwake na kitendo chake. Kwa hivyo anamuunga mkono kwa aliyoyasema kwa miujiza ya kushangaza, na Aya zilizo dhahiri, na amnusuru , na awaangushe anayemhalifu na kumfanyia uadui. Basi Je, ni ushahidi gani mkubwa zaidi kuliko ushahidi huu? Na kauli yake, "Na imefunuliwa kwangu Qur-ani hii ili kwayo niwaonye nyinyi na kila inayemfikia;" yaani, Mwenyezi Mungu aliniteremshia hii Qur-ani Tukufu kwa manufaa yenu na masilahi yenu. Kwamba niwaonye kwayo kutokana na adhabu chungu, na maonyo huwa kwa kutaja yale anayowaonya nayo kama vile kutia moyo, na vitisho, na kwa kubainisha vitendo na maneno ya nje na yaliyofichika ambayo mwenye kuyafanya, basi hakika atakuwa ameyakubali maonyo hayo. Basi Qur-ani hii ina maonyo kwenu, enyi mnaoongeleshwa, na kwa kila mwenye kufikiwa na Qur’ani hadi Siku ya Kiyama. Kwa maana, ndani yake kuna ubainisho wa kila matakwa ya kimungu yanayohitajiwa. Wakati Yeye Mtukufu alipobainisha ushahidi Wake, ambao ndio ushahidi mkubwa zaidi wa upweke wake, Akasema: Waambie hawa wanaopinga habari za Mwenyezi Mungu na kuwakadhibisha Mitume wake; "Je kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo." Yaani, wakishuhudia; basi usishuhudie wewe pamoja nao. Linganisha baina ya ushahidi wa msema kweli zaidi kati ya wasemao, na Mola Mlezi wa walimwengu wote, na ushahidi wa aliye safi zaidi katika viumbe vyote unaoungwa mkono na ushahidi wa uhakika, na hoja za wazi juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu peke yake asiyekuwa na mshirika. Na ushahidi wa wenye ushirikina ambao akili zao na dini zao zimepotoshwa, na maoni yao na maadili yao yameharibika; na ambao wamezicheka nafsi zao zenye akili, bali ushahidi wao umehalifu maumbile yao. Na kauli zao zilipingana katika kuthibitisha kwamba kuna miungu wengine pamoja na Mwenyezi Mungu, pamoja na kwamba hata fikira ndogo potofu haitokei kwa yale waliyoyahalifu; achilia mbali hoja mbalimbali. Na jichagulie mwenyewe ni upi kati ya huo ushahidi mbili ikiwa unatumia akili, na sisi tunajichagulia kile alichomchagulia Mwenyezi Mungu Nabii wake ambaye Mwenyezi Mungu alituamrisha tumwige. Kwa hivyo akasema, "Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu;" yaani, Yuko peke yake tu, na hakuna anayestahiki kuabudiwa wala uungu isipokuwa Yeye tu, kama vile Yeye yu peke yake katika uumbaji na uendeshaji. "Nami hakika niko mbali na mnaowashirikisha" naye miongoni mwa viabudiwavyo, na wenza, na kila kinachoshirikishwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi huu ndio uhakika wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu; kuthibitisha uungu kwa Mwenyezi Mungu na kuukanusha kwa asiyekuwa Yeye.