Al-An'aam
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
وَلَا تَقْرَبُوا۟ مَالَ ٱلْيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُۥ ۖ وَأَوْفُوا۟ ٱلْكَيْلَ وَٱلْمِيزَانَ بِٱلْقِسْطِ ۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَٱعْدِلُوا۟ وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ ٱللَّهِ أَوْفُوا۟ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ 152
{152} "Wala msiikaribie mali ya yatima" kwa kula au kuibadilishana kwa namna ya kujipa bure, au kuichukua bila ya sababu yoyote, "isipokuwa kile kilicho kizuri kabisa;" yaani, isipokuwa katika hali ambayo mali yao inabaki kuwa nzuri na wananufaika kwayo. Kwa hivyo, hili likaashiria kuwa hairuhusiwi kuikaribia kuitumia kwa njia inayowadhuru mayatima au kwa njia isiyokuwa na madhara wala manufaa; "mpaka afike" yatima huyo "utuuzima wake." Yaani, mpaka abaleghe na aweze kuwa wa kufanya uamuzi mzuri, na ajue namna ya kutenda mambo vyema. Kwa hivyo, anapofikia utuuzima wake, anapewa wakati huo mali yake, na inatumiwa chini ya uangalizi wake. Na katika hili kuna ishara ya kwamba yatima kabla ya kufikia utuuzima anazuiwa kusimamia mali yake, na kwamba mlezi wake anaendesha mali yake kwa kilicho bora zaidi kwake, na kwamba kuzuia huku kunaisha kwa kufikia utuuzima. "Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu;" yaani, kwa uadilifu na kutimika kukamilifu. Na mkifanya juhudi katika hayo, kwa bidii; basi "hatuibebeshi nafsi isipokuwa kwa uwezo wake." Yaani, kwa kiwango inavyoweza, wala hatuifanyii ugumu. Kwa hivyo, mwenye kufanya juhudi katika kutimiza kipimo cha wingi na cha uzito, kisha upungufu fulani ukapatikana kutoka kwake, lakini yeye hakupuuza katika hilo wala hakujua hilo, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu. Na kwa Aya hii [na mfano wake], wanazuoni wa Misingi ya Fiqh waliitumia kama ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu hamtwiki yeyote asichokiweza, na kwamba mwenye kumcha Mwenyezi Mungu katika yale aliyoyaamrisha na akafanya yale anayoweza katika hayo, basi hakuna ubaya juu yake katika yasiyokuwa hayo. "Na mnaposema" neno ambalo kwalo mnahukumu baina ya watu, na mnatenganisha mazungumzo baina yao, na mkazungumza kwalo kwa maneno na hali mbalimbali, "basi fanyeni uadilifu" katika kauli yenu kwa kuzingatia ukweli kwa yule mnayempenda na yule mnayemchukia, na uadilifu, na kutoficha kile kinachohitaji kubainishwa. Kwa maana, kuegemea dhidi ya yule unayemchukia kwa kusema juu yake au katika mazungumzo yake kuna dhuluma iliyoharamishwa. Bali mwanachuoni akizungumzia maneno ya watu wa uzushi katika dini, basi la wajibu kwake ni kumpa kila mwenye haki haki yake na kwamba kueleza yale yaliyo ndani yake ya haki na batili, na azingatie ukaribu wake na haki, na umbali wake kutoka kwayo. Na wanachuoni wa Fiqh walitaja kwamba kadhi inamlazimu awe mwadilifu baina ya wapinzani wawili katika mtazamo wake na kauli yake. "Na ahadi ya Mwenyezi Mungu,itimizeni." Na hili linajumuisha ahadi aliyowafungia waja wake kama vile kuzitekeleza haki zake na kuzitimiza, na pia ahadi wanayofunga viumbe baina yao. Basi hizo zote ni lazima kizitimiza, na ni haramu kuzibatilisha na kuzikiuka. "Hayo" yaliyotajwa miongoni mwa hukumu mbalimbali, "amewausia" [Mwenyezi Mungu] "kwayo ili mkumbuke" yale Aliyowabainishia miongoni mwa hukumu mbalimbali, na mtekeleze wasia wa Mwenyezi Mungu kwenu kama inavyostahiki, na mjue yale yaliyomo ya hekima na hukumu mbalimbali.