Al-An'aam
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
فَمَن يُرِدِ ٱللَّهُ أَن يَهْدِيَهُۥ يَشْرَحْ صَدْرَهُۥ لِلْإِسْلَـٰمِ ۖ وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُۥ يَجْعَلْ صَدْرَهُۥ ضَيِّقًا حَرَجًا كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِى ٱلسَّمَآءِ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْعَلُ ٱللَّهُ ٱلرِّجْسَ عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ 125
{125} Yeye Mtukufu anasema akiwabainishia waja wake alama ya furaha ya mja, na uongofu wake; na alama ya mshaka yake, na upotevu wake: Hakika yule ambaye kifua chake kuliufungukia Uislamu. Yaani, kunapanuka na kuwa na nafasi, kwa hivyo kikaangazwa na nuru ya imani, na kikahuishwa na mwangaza wa yakini. Kwa hivyo nafsi yake ikatulia kwa hilo, na akapenda heri, na nafsi yake ikatii ili afanye mema, akawa anapata ladha katika hilo, bila ya kuona uzito ndani yake. Basi hii ni alama ishara Mwenyezi Mungu amemuongoa na akamneemesha kwa kumwezesha kutenda mema, na kufuata njia iliyonyooka kabisa. Na kwamba alama ya yule ambaye mwenyezi Mungu anataka “kumpotosha” ni kwamba “hukifanya kifua chake kuwa kifinyu, kimebana.” Yaani, kinakuwa kifinyu mno katika kuwa na imani na elimu na yakini. Tayari moyo wake umezama ndani ya fikira potofu, na matamanio, basi hakuna kheri inayoufikia, wala haufunguki moyo wake kufanya heri. Kana kwamba kutokana na ufinyu wake na ugumu wake, unakaribia " anapanda katika mbingu." Yaani, ni kana kwamba ameelemewa na kupanda mbinguni ambako hakuna msaada wowote. Na hili ni kwa sababu ya kutoamini kwao;na hilo ndilo lililomfanya Mwenyezi Mungu kuwawekea uchafu juu yao. Kwa sababu walijifungia wenyewe mlango wa rehema na ihsani, na hii ndiyo mizani isiyopunja na njia isiyobadilika. Kwani mwenye kutoa, na akamcha Mwenyezi Mungu, na akasadiki yaliyo mema zaidi, Mwenyezi Mungu atamsahilishia yawe mepesi. Na ama mwenye kufanya ubahili na mwenye kujiona anajitosheleza, na akayakadhibisha yaliyo mema zaidi, basi atamrahisishia yawe magumu.