Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hashr
Surah 59

Al-Hashr

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 2

هُوَ ٱلَّذِىٓ أَخْرَجَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ مِن دِيَـٰرِهِمْ لِأَوَّلِ ٱلْحَشْرِ ۚ مَا ظَنَنتُمْ أَن يَخْرُجُوا۟ ۖ وَظَنُّوٓا۟ أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمْ حُصُونُهُم مِّنَ ٱللَّهِ فَأَتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا۟ ۖ وَقَذَفَ فِى قُلُوبِهِمُ ٱلرُّعْبَ ۚ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِى ٱلْمُؤْمِنِينَ فَٱعْتَبِرُوا۟ يَـٰٓأُو۟لِى ٱلْأَبْصَـٰرِ 2

{2} Na katika hayo kuna kumsaidia Mtume wake – Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – dhidi ya makafiri miongoni mwa Watu wa Kitabu kutoka kwa kabila la Banu An-Nadhir walipomfanyia hiyana Mtume wake, basi akawatoa majumbani mwao, na makazi yao waliyokuwa wameyazoea na kuyapenda. Kuwafukuza kwao huko kulikuwa kwenda Khaybar ndiko mkusanyiko wa kwanza na kufukuziliwa mbali na Mwenyezi Mungu kupitia mikono ya Mtume wake Muhammad Rehema na Amani zimshukie. Aya hii tukufu iliashiria kuwa watakuwa na mkusanyiko na kufukuziliwa mbali kusiokuwa huku. Hilo lilitokea wakati Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alipowahamisha kutoka Khaybar, na kisha Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, akawafukuza waliosalia humo. “Hamkudhani” enyi Waislamu “kuwa watatoka” kutoka katika maskani zao. Kwa sababu ya kutodhurika ugumu wa ngome zao, na ulinzi wake mkali, na nguvu zao ndani yake, “nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda dhidi ya Mwenyezi Mungu.” Basi wakafurahishwa nazo, na zikawadanganya, na wakadhania kuwa hawataweza kufikiwa humo, wala hakuna anayeziweza. Lakini uweza wa Mwenyezi Mungu uko nyuma ya hayo yote. Ngome na majumba marefu haviwezi kusimama mbele yake wala nguvu na ulinzi havifai chochote. Ndiyo maana akasema: “Lakini Mwenyezi Mungu akawafikia kwa mahali ambako hawakutazamia.” Na hilo ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Alitia uwoga mkubwa katika nyoyo zao.” Na hilo ndilo jeshi kubwa zaidi la Mwenyezi Mungu, ambalo wala idadi wala vifaa wala nguvu wala ukali havisaidii kitu mbele yake. Na jambo wanalolitarajia, na wanadhania kuwa litawajia kosa ikiwa likiwafikia ni ngome walizojikinga ndani yake, na ambazo nafsi zao zimetulia juu yake. Lakini mwenye kuwa na imani na asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi huyo ataachiliwa mbali bila msaada. Na mwenye kutegemea asiyekuwa Mwenyezi Mungu, alilotegemea hilo linakuwa balaa kubwa kwake. Kwa hivyo, wakajiwa na jambo kutoka mbinguni lililoingia katika nyoyo zao, ambazo ndizo mahali pa uthabiti na subira, au udhaifu. Basi akawaondolea nguvu na ukali wao, na akawaacha na udhaifu na woga ambavyo hawakuwa na hila ya kuvizuilia. Na kwa hilo akawa amemsaidia Mtume dhidi yao. Ndiyo maana akasema: “Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya Waumini.” Hayo ni kwa sababu walifanya suluhu na Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa sharti ya kwamba wataruhusiwa kuchukua kile ambacho ngamia wataweza kubeba. Kwa hivyo, wakavunja dari zao nyingi walizokuwa wanazipenda mno, na wakawapa mamlaka Waumini kwa sababu ya uasi wao, ili waziharibu nyumba zao na wazibomoe ngome zao. Kwani wao ndio waliojifanyia ubaya wenyewe na wakawa ni msaada mkubwa dhidi yao wenyewe. “Basi zingatieni enyi wenye macho!” Yaani, wenye macho ya kuona sawasawa na akili kamili. Kwani katika hili kuna mazingatio ambayo kwayo yanajulikana matendo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika wale wanaoipinga haki, wale wanaofuata matamanio yao, ambao kiburi hakikuwafaa kitu, wala nguvu zao hazikuwazuilia kitu, wala ngome zao hazikuwalinda kwa chochote. Wakati jambo la Mwenyezi Mungu lilipowajia mateso yaliwafikia kwa sababu ya dhambi zao, na lililo muhimu ni maana ya jumla, siyo sababu mahususi. Kwa maana, aya hii inaashiria amri ya kuzingatia, ambayo ni kuzingatia kitu sawa na chenzake, kulinganisha kitu na kile kinachofanana nacho, na kutafakari juu ya maana na hekima zilizomo katika hukumu mbalimbali, ambazo ndizo mahali pa akili na kufikiria. Na kwa hayo, akili hukamilika, ufahamu hutiwa nuru, imani huongezeka, na ufahamu wa kweli hupatikana.