Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Hashr
Surah 59

Al-Hashr

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 10

وَٱلَّذِينَ جَآءُو مِنۢ بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا ٱغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَٰنِنَا ٱلَّذِينَ سَبَقُونَا بِٱلْإِيمَـٰنِ وَلَا تَجْعَلْ فِى قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ رَبَّنَآ إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ 10

{10} Aina hizi mbili bora safi ni maswahaba watukufu na maimamu wakubwa, waliopata tangulia, fadhila mbalimbali, sifa mbalimbali walizopata walizotangulia kwazo wale waliokuja baada yao na wakawafikia kwazo wale waliokuwa kabla yao, na wakawa waumini wakweli, mabwana wa Waislamu, na viongozi wa wacha Mungu, na inatosha wale waliokuja baada yao kuwa na fadhila ya kutembelea nyuma yao na kuufuata uwongofu wao, na ndiyo sababu Mwenyezi Mungu akataja miongoni mwa watakaofuata wale wanaofuatwa, [na kutembelea nyuma yao], akasema: “Na wale waliokuja baada yao.” Yaani, baada ya Muhajirina na Ansari, “wanasema” kwa njia ya kujinasihi wenyewe na kunasihi Waumini wengine wote: “Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani.” Hii ni dua inayowajumuisha Waumini wote katika wale waliotangulia miongoni mwa masahaba na wale waliokuwa kabla yao na baada yao, na hizi ni miongoni mwa fadhila za imani; kwamba Waumini wananufaika wao kwa wao na wanaombeana wao kwa wao; kwa sababu ya kushirikiana kwao katika imani, jambo linalohitaji kuwepo mafungamano ya udugu baina ya waumini, ambao katika matawi yake ni kuombeana dua wao kwa wao, na kupendana, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akataja katika dua hii kuondolewa kwa chuki kutoka moyoni, ikijumuisha ndogo na nyingi, ambayo ikiwa haitakuwepo, basi kinyume chake kinathibiti, ambacho ni mapenzi baina ya waumini, kulindana, kushauriana, na mambo mengine ambayo ni miongoni mwa haki za waumini. Basi Mwenyezi Mungu akawasifu wale waliokuwa baada ya maswahaba kwamba wana imani, kwa sababu kauli yake: “waliotutangulia kwa Imani” ni ishara kwamba wanashirikiana katika hilo, na kwamba wao ni wafuasi wa Maswahaba katika itikadi za imani na misingi yake, na wao ni watu wa Sunna na umoja ambao sifa hii kamili haiwezi kuwa kwa wengine isipokuwa wao tu, na akawaelezea kwamba wanakiri dhambi na kuomba msamaha kwa sababu yake, na kuombeana msamaha, na kujitahidi kuondoa chuki na kinyongo [katika nyoyo zao] dhidi ya ndugu zao waumini; kwa sababu kuomba kwao haya kunahitajia haya tuliyoyataja na kunajumuisha kupendana wao kwa wao, na kwamba kila mmoja anampendea ndugu yake kile anachojipendea mwenyewe, na kwamba ampe nasaha anapokuwepo na hata kama hayupo, kama yu hai na kama amekufa. Aya hii tukufu inaashiria kwamba hizi ni miongoni mwa haki za waumini wao kwa wao. Kisha wakahitimisha dua yao kwa majina mawili matukufu ya Mwenyezi Mungu yenye kuashiria ukamilifu wa rehema ya Mwenyezi Mungu na ukubwa wa huruma yake na wema wake kwao, ambayo ni pamoja na: Bali, [katika] kubwa yake zaidi ni kuwawezesha kutekeleza haki zake na haki za waja wake. Aina hizi tatu ni aina za umma huu, nao wale wanaostahiki ngawira iliyopatikana bila vita, ambayo matumizi yake yanarudi kwenye masilahi ya Uislamu, na hawa ndio watu wake ambao ndio watu wake, Mwenyezi Mungu atufanye miongoni mwao kwa neema yake na ukarimu wake.