Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Mujaadila
Surah 58

Al-Mujaadila

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 5

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ كُبِتُوا۟ كَمَا كُبِتَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَقَدْ أَنزَلْنَآ ءَايَـٰتٍۭ بَيِّنَـٰتٍ ۚ وَلِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابٌ مُّهِينٌ 5

Kuna hukumu kadhaa katika aya hizi: Miongoni mwake ni upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake na utunzaji wake kwao. Ambapo alitaja malalamiko ya mwanamke huyu aliyeteseka, akayaondoa, na akamwondolea balaa. Bali aliiondoa balaa hii kwa hukumu yake ya ujumla kwa kila mtu ambaye atakuwa katika suala kama hili. Na miongoni mwake ni kwamba kumfananisha mke na mama ya mtu ni jambo linalohusiana na mke peke yake, kwa sababu Mwenyezi Mungu alisema: "wake zao." Na ikiwa hilo lingeharamisha kijakazi wake pia, basi hilo halingakuwa dhihar (yaani, kumfananisha mke na mama ya mtu katika uharamu), bali litakuwa ni katika aina moja na kuharamisha vitu vizuri kama vile vyakula na vinywaji, ambalo mtu anapaswa kutoa kafara ya kuapa tu. Na miongoni mwake haiwi sahihi kumfanyia mwanamke dhihar (kumsawazisha na mama ya mtu) kabla ya kumuoa. Kwa sababu bado hajaingia katika wake zake wakati huo, kama vile kumtaliki hakuwi sahihi, sawa alikwisha amua hilo au alilifungamanisha na kitu fulani. Na miongoni mwake ni kwamba dhihar (mtu kumsawazisha mkewe na mama yake) ni haramu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliliita hilo, "neno ovu mno, na la uongo." Na miongoni mwake ni kwamba Mwenyezi Mungu alitanabahisha juu ya hukumu na hekima yake. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisema: “Hao si mama zao." Na miongoni mwake ni kwamba inachukiza kwa mwanaume kumwita mkewe kwa jina la maharimu wake. Kama vile kusema: 'Ewe mama yangu, ewe dada yangu" na mfano wa hayo. Kwa sababu hayo yanafanana na kile kilichoharamishwa. Na miongoni mwake ni kwamba kafara inalazimu anaporudia mwanamume huyo yale aliyojiharamishia, kulingana na kauli mbili tofauti zilizoko, na wala haiwi lazima kwa kujiharamishia huko tu. Na miongoni mwake ni kwamba inatosha katika kafara kutoa huru mtumwa mdogo, au mzee, au mwanamume, au mwanamke. Kwa sababu aya hii haikuwekea hilo kitu mahususi. Na miongoni mwake ni kwamba ni lazima ilipwe kafara hivyo ikiwa ni kumtoa mtumwa utumwani, au kufunga saumu kabla ya kujamiiana. Kama Mwenyezi Mungu alivyoamrisha iwe hivyo. Hii ni tofauti na kafara ya kulisha, ambayo inaruhusika kujamiiana hata kama haijaisha. Na miongoni mwake ni kwamba labda hekima iliyo nyuma ya ufaradhi wa kutoa kafara hii kabla ya kujamiiana ni kwamba hilo linapelekea zaidi kuitoa. Kwa sababu, ikiwa atatamani sana ngono na anajua kuwa hataruhusiwa hilo ila baada ya kutoa kafara, ataharakisha kuitoa. Na miongoni mwake ni kwamba ni lazima kuwalisha watu masikini sitini. Na kama atakusanya chakula cha masikini sitini na akampa mmoja wao au zaidi wanaopungua sitini, hilo halitakubaliwa. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisema: "Basi awalishe masikini sitini."

{5} Kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kuwaasi, hasa kwa mambo ya kutisha kama vile kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa ukafiri na kuwafanyia uadui vipenzi wa Mwenyezi Mungu. Na kauli yake: "watadhalilishwa kama walivyodhalilishwa wale waliokuwa kabla yao" ili yawe malipo mwafaka, wala hawatakuwa na hoja yoyote dhidi ya Mwenyezi Mungu. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu alikwisha simamisha hoja yake ya kukata juu ya viumbe, na aliteremsha ishara zilizo wazi na hoja zinazobainisha uhakika wa mambo, na kuweka wazi makusudio. Kwa hivyo, mwenye kuzifuata na akazifanyia kazi, basi huyo ni miongoni mwa walioongoka, waliofaulu. "Na makafiri" wanaoyakufuru hayo, "watapata adhabu ya kufedhehesha." Kama vile walivyokuwa wakizidhalilisha ishara za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atawadunisha na kuwadhalilisha.