Az-Zukhruf
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
وَسْـَٔلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَآ أَجَعَلْنَا مِن دُونِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ءَالِهَةً يُعْبَدُونَ 45
{45} "Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: 'Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rahmani'" ili washirikina wawe na hoja fulani ambayo wanamfuata kwayo yeyote miongoni mwa Mitume. Kwa maana ukiwauliza na kufuatilia hali zao, hutapata yeyote miongoni mwao anayelingania kuchukua mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, na kwamba Mitume wote, kuanzia wa mwanzo wao hadi wa mwisho wao walilingania kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, bila mshirika. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: "Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Twaghut (Shetani na vyote vinavyoabudiwa visivyokuwa Mwenyezi Mungu)." Na kila Mtume aliyetumwa na Mwenyezi Mungu alikuwa akiwaambia umma wake, "Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye." Basi hilo likaashiria kwamba washirikina hawana msingi wowote wa kuunga mkono ushirikina wao, si wa aina ya kiakili iliyo sahihi, wala wa kimaandiko kutoka kwa Mitume.