An-Nisaa
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ يُحَرِّفُونَ ٱلْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِۦ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَٱسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَٰعِنَا لَيًّۢا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِى ٱلدِّينِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُوا۟ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَٱسْمَعْ وَٱنظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَـٰكِن لَّعَنَهُمُ ٱللَّهُ بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا 46
{46} Kisha akaeleza jinsi upotevu wao na ukaidi wao, na kupendelea kwao batili kuliko haki. Akasema, "Miongoni mwa Mayahudi" Yani Mayahudi, nao ni wanachuoni wa upotovu miongoni mwao wamo "wanaopotosha maneno kuyatoa pahali pake." Ima kwa kubadilisha maneno au maana, au yote mawili. Na katika upotoshaji wao ni kuzichukulia sifa ambazo zilitajwa katika vitabu vyao ambazo haziingiani wala hazisadikiki isipokuwa kwa Muhammad – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kwamba si yeye aliyemaanishwa kwazo wala aliyekusudiwa kwazo. Bali alikusudiwa kwazo asiyekuwa nayo. Na wakalificha hilo. Basi hiyo ndiyo hali yao katika elimu, ambayo ndiyo hali mbaya mno. Waligeuza uhakika ndani yake, na wakaichukulia haki kuwa ndiyo batili; kwa hivyo wakaikanusha haki kwa sababu ya hilo. Na ama hali yao katika matendo na kufuata, wao hakika "husema: Tumesikia na tumeasi" Yani: Tumesikia kauli yako na tukaasi amri yako. Na huu ndio ukafiri wa hali ya juu zaidi, na ukaidi, na kupotea mbali na utiifu. Na vile vile wanamwongelesha Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa kauli mbaya zaidi, na iliyo mbali zaidi na adabu. Kwa hivyo wao husema, "sikia bila ya kusikilizwa" wakikusudia: Sikia kutoka kwetu, bila ya kusikilizwa yale unayopenda, bali yale unayochukia. "Na Raai'naa" [Na] kusudio lao kwa hilo neno "Raai'naa" likiwa kumtia dosari mbaya, na wakadhania kuwa usemi huo kwa kuwa unaweza kumaanisha yale ambayo hawakukusudia miongoni mwa mambo kwamba litaonekana kuwa zuri kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa hivyo, wakafikia kwa kauli hiyo ambayo kwayo wanageuza ndimi zao kukashifu Dini na kumtukana Mtume. Na wanasema hayo waziwazi baina yao. Ndiyo maana akasema, "kwa kuzipotoa ndimi zao na kuitukana Dini," kisha akawaelekeza katika yale yaliyo bora kwao kuliko hayo. Akasema, "Na lau kama wangelisema: Tumesikia na tumetii, na usikie na "Undhurna (Utuangalie)", ingelikuwa heri kwao na ya unyoofu zaidi." Na hayo ni kwa sababu ya yale yaliyojumuishwa na maneno haya ya kauli njema na adabu zinazofaa katika kumwongelesha Mtume, na kuifuata amri yake, na uzuri wa upole wao katika kutafuta kwao elimu kwa kusikiliza swali lao na kulitunza jambo lao. Hivi ndivyo wanavyopaswa kutenda. Lakini kwa vile maumbile yao ya asili hayakuwa safi, wakayapa hayo mgongo, na Mwenyezi Mungu akawafukuza kwa ukafiri wao na ukaidi wao, na kwa sababu ya hayo akasema, "Lakini Mwenyezi Mungu aliwalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini isipokuwa wachache tu."