Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Surah 4

An-Nisaa

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 176

يَسْتَفْتُونَكَ قُلِ ٱللَّهُ يُفْتِيكُمْ فِى ٱلْكَلَـٰلَةِ ۚ إِنِ ٱمْرُؤٌا۟ هَلَكَ لَيْسَ لَهُۥ وَلَدٌ وَلَهُۥٓ أُخْتٌ فَلَهَا نِصْفُ مَا تَرَكَ ۚ وَهُوَ يَرِثُهَآ إِن لَّمْ يَكُن لَّهَا وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَتَا ٱثْنَتَيْنِ فَلَهُمَا ٱلثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَ ۚ وَإِن كَانُوٓا۟ إِخْوَةً رِّجَالًا وَنِسَآءً فَلِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ ٱلْأُنثَيَيْنِ ۗ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمْ أَن تَضِلُّوا۟ ۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌۢ 176

{176} Mwenyezi Mungu Mtukufu alijulisha kwamba watu walimuuliza Mtume wake – rehema na amani ziwe juu yake – hukumu ya kisheria kuhusiana na Kalala. Hii ni kwa ushahidi wa kauli yake, "sema: Mwenyezi Mungu anawapa hukumu ya kisheria juu ya kalala.” Naye ni maiti anayekufa na hana wana wa kutoka kwa mgongo wake, wala mwana wa mwana wa kiume, na baba, wala babu. Na ndiyo maana akasema, "Ikiwa mtu amekufa, naye hana mwana," yaani, hakuna wa kiume wala wa kike, wala mwana wa kutoka katika mgongo wake wala mwana wa mwana wa kiume. Na vile vile, ikiwa hana baba kwa Ushahidi kwamba aliwarithisha kaka na madada kwa pamoja hawarithi wakiwa pamoja na baba. Basi akifa ilhali hana mwana wala baba, "lakini anaye dada," yaani, wa kwa baba na mama, au wa kwa baba tu, na sio wa kwa mama kwa kuwa hukumu Yake ilikwisha tangulia. "Basi huyo atapata nusu ya alichokiacha," yaani nusu cha alichoacha kaka yake. Kama vile pesa, na mali isiyohamishika, na vyombo, na visivyokuwa hivyo. Na hilo ni baada ya deni na wasia kama ilivyotangulia. "Naye," yaani, kaka yake wa kwa baba na mama au wa kwa baba tu, "atamrithi" (dada yake) ikiwa hana mwana." Na wala hakuwekewa urithi maalumu kwa sababu yeye hukuchua chote kilichosalia, basi atachukua mali yake yote ikiwa hakuna mrithi mwenye kifungu maalum si anayeshiriki naye au atachukua kile kilichoachwa na mafungu ya urithi. "Na ikiwa wao ni madada wawili," na zaidi, "basi watapata theluthi mbili za alichokiacha. Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake," yaani, ikiwa wa kiume na wa kike ambao si wa kwa mama watajumuika. "Basi wa kiume atapata sehemu iliyo sawa na ya wa kike wawili." Basi fungu la wa kike linaanguka, na kaka zao wanachukua mafungu mawili ya kwa wa kike mmoja. "Mwenyezi Mungu anawabainishia ili msipotee." Yaani, anawabainishia hukumu zake mnazohitaji, na anawawekea wazi na anawaelezea kutokana na fadhila zake na wema wake, ili muongoke kwa ubainisho wake [na mfanyie kazi] hukumu zake. Na ili msipotee kutoka katika Njia iliyonyooka, kwa sabbau ya ujinga wenu na kutojua kwenu. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu." Yaani, anayajua ya ghaibu na ya dhahiri, na mambo yaliyopita na yajayo, na Anajua haja zenu juu ya kubainishiwa kwake, na kuwafundisha kwake, kwa hivyo Anawafundisha kutoka katika elimu yake ambayo itawafaa daima katika kila nyakati na mahali popote. Mwisho wa Tafsiri ya Surat An-Nisa. Basi Sifa njema na shukrani ni za Mwenyezi Mungu.