An-Nisaa
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
وَيَسْتَفْتُونَكَ فِى ٱلنِّسَآءِ ۖ قُلِ ٱللَّهُ يُفْتِيكُمْ فِيهِنَّ وَمَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فِى ٱلْكِتَـٰبِ فِى يَتَـٰمَى ٱلنِّسَآءِ ٱلَّـٰتِى لَا تُؤْتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرْغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلْوِلْدَٰنِ وَأَن تَقُومُوا۟ لِلْيَتَـٰمَىٰ بِٱلْقِسْطِ ۚ وَمَا تَفْعَلُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِهِۦ عَلِيمًا 127
{127} Fatwa ni Muulizaji kumuuliza anayeulizwa kubainisha hukumu ya kisheria kuhusiana na hilo alilouliza juu yake. Kwa hivyo, akajulisha kuhusu Waumini kwamba wanamuuliza Mtume - rehema na amani zimshukie - fatwa kuhusu hukumu ya wanawake inayohusiana nao. Basi Mwenyezi Mungu akachukua usimamizi wa fatwa hii, na akasema, "Sema: Mwenyezi Mungu anawatolea fatwa juu yao." Basi fanyeni kazi kulingana na aliyokupa fatwa katika mambo yote ya wanawake, kuhusiana na kuwatimizia haki zao na kujiepusha kuwadhulumu kwa ujumla na katika mambo maalum. Na hii ni amri ya jumla inayojumuisha yale yote ambayo Mwenyezi Mungu ameyaweka kama sheria, maamrisho na makatazo kuhusiana na wanawake, wake na wengineo, wadogo na wakubwa. Kisha baada ya kuijumlisha amri hiyo, akabainisha kimahsusi amri kwa wanyonge, kama vile mayatima na watoto wadogo kwa sababu ya kuwajali na kuwakemea katika kupuuza haki zao. Na akasema, "na yale mnayosomewa katika Kitabu hiki kuhusu mayatima wanawake." Yani, Yeye pia anawapa fatwa kuhusiana na msomewayo katika Kitabu kuhusu mambo ya mayatima wanawake, "ambao hamuwapi kile walichoandikiwa;" na huku ni kupeana habari juu ya hali iliyopo kwa hakika wakati huo. Kwa maana yatima anapokuwa chini ya ulezi wa mwanamume; anampunja haki yake na anamdhulumu, ima kwa kula mali yake ambayo ni yake yatima au baadhi yake, au kumzuia asiolewe ili anufaike kwa mali yake kwa kuhofia kuitoa katika mikono yake ikiwa atamwozesha au kuichukua kutoka kwa shemeji yake ambaye atamwoa kwa sharti au kwa kinginecho. Hili ni ikiwa hamtaki, au anamtaka hali ya kuwa ana uzuri na mali na hampi mahari yake kwa uadilifu, bali anampa kidogo kuliko anachostahili. Basi Yote haya ni dhuluma inayoingia chini ya andiko hili, na ndiyo maana akasema, "na mnapenda kwamba muwaoe." Yan,i hamtaki kuwaoa au mnataka kuwaoa kama tulivyotaja mfano wake. "Na wanyonge miongoni mwa watoto," Yaani, anakupa fatwa kuhusu wanaodhulumiwa miongoni mwa watoto wadogo, kwamba uwape haki zao katika mirathi na mambo mengine; na kwamba usichukue mali zao mbele ya dhuluma na kiholela. "Unawafanyia haki mayatima;" yaani, kwa uadilifu kamili, na hii ni pamoja na kuwasimamia kwa kuwajibisha kutimiza amri ya Mwenyezi Mungu na yale aliyowajibisha juu ya waja wake. Hivyo, mawalii wanawajibikiwa na hayo, na kuwajibisha kufanya yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu. Hii ni pamoja na kuwasimamia katika maslahi yao ya kidunia kwa kuendeleza mali zao na kuwatafutia heri zaidi, na kutokurubia ila kwa yaliyo bora. Na hali kadhalika, hawaonyeshi upendeleo kwao rafiki na si mwengine katika ndoa na wengine ili kutimiza haki zao. Na hii ni kutokana na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake. Ambapo alisisitiza sana kujali maslahi ya wale ambao hawajijali kutokana na udhaifu wao na kufiwa na baba yake. Kisha akahimiza juu ya wema kwa ujumla, na akasema, "Na chochote mnachofanya katika heri," kwa mayatima na wengineo, ikiwa kheri ni ya kupita au ya lazima, "Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hayo." Yaani, ujuzi wake unajumuisha kazi ya wale wanaofanya kazi kwa wema, ikiwa ni ndogo au kubwa, nzuri au mbaya, kwa hivyo humlipa kila mmoja kulingana na matendo yake.