Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Surah 4

An-Nisaa

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 11

يُوصِيكُمُ ٱللَّهُ فِىٓ أَوْلَـٰدِكُمْ ۖ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ ٱلْأُنثَيَيْنِ ۚ فَإِن كُنَّ نِسَآءً فَوْقَ ٱثْنَتَيْنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَ ۖ وَإِن كَانَتْ وَٰحِدَةً فَلَهَا ٱلنِّصْفُ ۚ وَلِأَبَوَيْهِ لِكُلِّ وَٰحِدٍ مِّنْهُمَا ٱلسُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُۥ وَلَدٌ ۚ فَإِن لَّمْ يَكُن لَّهُۥ وَلَدٌ وَوَرِثَهُۥٓ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ ٱلثُّلُثُ ۚ فَإِن كَانَ لَهُۥٓ إِخْوَةٌ فَلِأُمِّهِ ٱلسُّدُسُ ۚ مِنۢ بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِى بِهَآ أَوْ دَيْنٍ ۗ ءَابَآؤُكُمْ وَأَبْنَآؤُكُمْ لَا تَدْرُونَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ لَكُمْ نَفْعًا ۚ فَرِيضَةً مِّنَ ٱللَّهِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا 11

Aya hizi na Aya iliyo mwisho wa sura hii ni Aya za mirathi ambazo zinaijumuisha. Hizi pamoja na hadithi ya Abdullah bin Abbas, iliyothibiti katika Sahih Al-Bukhari. “Zifikisheni mirathi kwa wale wanaozistahiki. Na chochote chenye kubaki, basi ni cha mtu wa kiume anayestahiki zaidi;" zinajumuisha sehemu kubwa ya hukumu za mirathi, bali hukumu zote, kama utakavyoliona hilo, isipokuwa urithi wa akina nyanya. Huo haukutajwa ndani yake. Lakini ilithibiti katika “As-Sunan (vitabu vya hadithi) kutoka kwa Al-Mughirah bin Shu’bah na Muhammad bin Maslama: kwamba Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - alimpa nyanya sudusi moja, pamoja na makubaliano ya wanazuoni juu ya hilo.

{11} Basi kauli yake Yeye Mtukufu, "Mwenyezi Mungu anawausia juu ya watoto wenu." Yani, watoto wenu, enyi kundi la wazazi ni amana kwenu ambayo Mwenyezi Mungu amewausia kuyasimamia masilahi yao ya kidini na ya kidunia. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu, "Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu ktokana na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe." Basi watoto kwa wazazi ni wausiwa. Kwa hivyo, ima wautekeleze wasia huo, na wawe na thawabu nyingi. Au waupuuze, na wastahili onyo na adhabu. Na hii ni katika yale yanayoashiria kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye Mwingi wa huruma zaidi kwa waja wake kuliko wazazi, kwa kuwa aliwausia wazazi pamoja na ukamilifu wa huruma yao kwao. Kisha akataja namna ya urithi wao, akasema. "Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili." Yani, watoto kutoka katika kiuno, na watoto wa mtoto wa kiume, mwanamume ana mfano wa fungu la wanawake wawili ikiwa hakuna yule anayerithi fungu maalum pamoja nao, au kile ambacho kinabakishwa na mafungu maalumu wao wanagawanyiwa hicho namna hiyo. Na wanachuoni wamekubaliana kwa kauli moja juu ya hilo, na kwamba pamoja na uwepo wa watoto wa kutoka katika kiuno, basi urithi ni wao, na wana wa mwana hawana kitu, ambapo wana wa kiuno ni wa kiume na wa kike. Hii ni ikiwa watakusanyika wana wa kiume na wana wa kike. Na hapa kuna hali mbili: Wana wa kiume peke yao, na itakuja hukumu ya hali hii. Na wana wa kike peke yao. Na iliitaja hali hii kwa kauli yake, "Na wakiwa ni wanawake zaidi ya wawili" Yani, mabinti wa kutoka kwa kiuno, au mabinti wa wana wa kiume, watatu au zaidi. "Basi wana theluthi mbili za alichokiacha. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja" yani, binti ya maiti au binti wa mwana wa maiti. "Basi fungu lake ni nusu" Na haya ndiyo makubaliano ya wanachuoni. Imebakia isemwe: Je, inatoka wapi kwamba mabinti wawili wanastahiki theluthi mbili baada ya kuwepo kwa Ijmaa (makubaliano) juu ya hilo? Jibu ni kuwa inatokana na kauli yake, "Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu." Ambayo maana yake isiyokuwa ya moja kwa moja ni kwamba ikiwa watazidi mmoja, basi fungu linatoka kwa nusu, kisha hakuna chochote baada yake isipokuwa theluthi mbili tu. Na pia, kauli yake, "Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili" akiacha mwana wa kiume na binti. Basi mwana wa kiume ana theluthi mbili. Na Mwenyezi Mungu alisema kuwa ni kama fungu la wanawake wawili. Basi hilo likaonyesha kwamba mabinti wawili wana theluthi mbili. Na pia, ikiwa binti anapochukua theluthi moja pamoja na kaka yake, ilhali yeye ni mwenye kumdhuru zaidi kuliko dada yake, basi yeye dada kuichukua (yani theluthi moja) pamoja na dada yake ni katika mlango unaostahiki na unaofaa zaidi. Na pia, kauli yake Yeye Mtukufu kuhusu dada wawili; "Na wakiwa ni wanawake zaidi ya wawili, basi wana theluthi mbili za alichokiacha" ni andiko la moja kwa moja kuhusu madada wawili. Kwa hivyo, ikiwa madada wawili pamoja na umbali wao wanachukua theluthi mbili, basi mabinti wawili pamoja na ukaribu wao ni katika mlango unaostahiki zaidi na unaofaa zaidi (kuzichukua). Na Nabii - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - aliwapa mabinti wa Sa'd theluthi mbili, kama ilivyo katika vitabu vya hadithi sahihi. Inabakia isemwe: Ni nini faida katika kauli yake, "zaidi ya wawili"? Itasemwa: Faida katika hayo - na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi - ni kwamba ili ifahamike kwamba fungu ambalo ni theluthi mbili, haliongezeki kwa kuongezeka kwao juu ya wawili. Bali ni kuanzia wawili kwenda juu. Na Aya hii tukufu iliashiria kwamba ikiwa kutakuwa na binti mmoja tu wa kutoka katika kiuno, na binti wa mtoto wa kiume, au mabinti wa mwana wa kiume, basi binti wa kutoka kwa kiuno ana nusu. Na inabaki sudusi tu katika theluthi mbili ambazo Mwenyezi Mungu aliwawekea mabinti au mabinti za mwana wa kiume, na hiyo anapewa binti wa mwana wa kiume, au mabinti za mwana wa kiume. Na kwa sababu hii, sudusi hii inaitwa kuwa ni ya kukamilisha zile theluthi mbili. Vivyo hivyo, ni binti wa mwana wa kiume pamoja na mabinti za mwana wa kiume ambao wako chini zaidi yake. Na Aya pia inaashiria kwamba pindi mabinti au mabinti wa mwana wa kiume wanapochukua theluthi mbili zote, basi yeyote aliye chini yao anaanguka bila ya wao miongoni mwa mabinti za mwana wa kiume. Kwa sababu, Mwenyezi Mungu hakuwawekea fungu isipokuwa theluthi mbili tu, na tayari imeshatimia. Na kama ikiwa hawaanguki, basi inalazimu kwamba wapewe fungu zaidi ya theluthi mbili. Na hilo ni kinyume na andiko. Na hukumu zote hizi zimeafikiwa kwa kauli moja na wanachuoni. Na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu. Na kauli yake, "katika kile alichokiacha" iliashiria kuwa warithi wanarithi kila kitu alichokiacha maiti kama vile mali isiyohamishika, na vyombo, na dhahabu, na fedha na visivyokuwa hivyo. Hata pesa za damu ambazo hazikuwajibika isipokuwa baada ya kifo chake, na hata madeni yaliyo katika dhima yake. Kisha akataja urithi wa wazazi wawili, na akasema, "Na kwa wazazi wake wawili," yani, baba yake na mama yake. "Kila mmoja wao apate sudusi ya alichokiacha, ikiwa ana mtoto." Yani, mwana wa kutoka kwa kiuno au mwana wa mwana wa kiume sawa awe wa kiume au wa kike, mmoja au wengi. Ama mama, yeye hapati zaidi ya sudusi moja pamoja na yeyote katika watoto (wa maiti). Na ama baba, basi akiwa pamoja na (watoto wa maiti) wana wa kiume miongoni mwao, yeye hastahiki zaidi ya sudusi moja. Na ikiwa mtoto ni mwanamke au wanawake, na hakuna chochote kilichobaki baada ya mafungu yao maalum, kama vile wazazi wawili na mabinti wawili, basi baba hatapata kwa namna ya kuchukua kitu kilichobaki. Lakini ikiwa kuna kitu kilichobaki baada ya fungu la binti au mabinti, baba atachukua sudusi kwa namna ya fungu maalumu, na kilichobaki kwa kukichukua chote. Kwa sababu, tuliwapa watu wa mafungu maalum mafungu yao, na kilichobaki, basi ni cha mtu wa kiume anayesatahiki zaidi. Naye (baba) ndiye anayestahiki zaidi kuliko kaka, na ami na wasiokuwa hao. "Na akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wakawa wanamrithi, basi mama yake atapata theluthi moja" yani, na chenye kubaki, hicho ni cha baba. Kwa sababu, aliifungamanisha mali hii na baba na mama kufungamanisha kumoja, kisha akakadiria fungu la mama, kwa hivyo hilo likaashiria kuwa chenye kubaki ni cha baba. Na ilijulikana katika hilo kuwa baba asiyekuwa pamoja na watoto hana fungu maalum, bali anarithi kwa kuchukua kinachobaki chote, au kile kinachobakishwa na mafungu maalum. Lakini ikiwa mmoja wa wanandoa wawili atapatikana pamoja na wazazi wawili - na hili huwa linaitwa Al-'Umariyyayni, - basi mume au mke atachukua fungu lake, kisha mama atachukua theluthi moja ya kilichobakia, naye baba atachukia chenye kusalia. Na hilo liliashiriwa na kauli yake Yeye Mtukufu, "na wazazi wake wawili wakawa wanamrithi, basi mama yake atapata theluthi moja;" yani, theluthi ya kile walichorithi wazazi wawili. Nacho katika sura hizi mbili: ima ni sudusi katika mume, na mama, na baba, au robo katika mke, na mama, na baba. Na Aya hii haikuashiria kwamba urithi wa mama ni theluthi kamili ya mali pasi na kuwepo watoto mpaka isemwe: Kwamba sura mbili hizi hazijajumuishwa kwenye hili. Na inaeleza hilo kwamba kile ambacho mume au mke anachochukua ni sawa na kile ambacho wadai huchukua. Kwa hivyo inakuwa kutoka kwa rasilmali. Nayo inayobaki inakuwa kati ya wazazi wawili. Na kwa sababu ikiwa tutampa mama theluthi moja ya mali, italazimu amzidi baba katika suala la mume, au baba achukue ziada kiasi cha nusu ya sudusi katika suala la mke. Na hili halina mfano wake. Kwani, kinachojulikana ni yeye (mama) kutoshana na baba, au yeye (baba) kuchukua mara mbili ya kile anachochukua mama. "Na akiwa ana ndugu, basi mama yake atapata sudusi." Nao ni ndugu kwa baba na mama, au wa kwa mama, sawa wawe wa kiume au wa kike, wawe wanarithi au waliozuiliwa kurithi na baba au babu. Lakini inaweza kusemwa: Maana ya dhahiri ya kauli yake, "Na akiwa ana ndugu" haijumuishi wasiorithi, kwa ushahidi wa kwamba haiwaingizi wale waliozuiliwa na nusu. Na kwa kuzingatia hili, hatamzuia kupata theluthi moja isipokuwa ndugu wanaorithi. Na hili linaungwa mkono na ukweli kwamba hekima ya kuwazuia theluthi ni kwa ajili kuwapa kitu katika mali, nayo haipo. Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi. Lakini kwa sharti ya kuwa wawe wawili au zaidi. Na hilo linaletewa shida kwa sababu ya kuja kwa neno 'ndugu' katika wingi. Na hilo lilijibiwa kwamba inawezekana kutumia wingi lakini ukakusudiwa uwili, kama katika kauli yake Mtukufu kuhusu Daud na Sulaiman, "Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo." Na akasema kuhusu ndugu wa kwa mama; "Na ikiwa mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye kaka au dada, basi kila mmoja kati yao ana sudusi. Na wakiwa zaidi kuliko hivyo, basi watashirikiana katika theluthi." Kwa hivyo akatumia neno la wingi, ingawa kilichokusudiwa kwalo ni wawili au zaidi kwa kauli moja. Na kwa mujibu wa hili, ikiwa ataacha nyuma mama, na baba, na kaka zake, basi mama atapata sudusi, na chenye kubaki ni cha baba, kwa hivyo wakawa wamezuia mama kupata theluthi pamoja na kwamba baba aliwazuia, isipokuwa kwa uwezekano ule mwingine. Kwani, mama atapata theluthi, na chenye kubaki ni cha baba. Kisha Yeye Mtukufu akasema, "baada ya wasia iliyousiwa au kulipa deni." Yani, faradhi hizi, na mafungu haya, na mirathi vinatokea na vinastahiki baada ya kutolewa kwa madeni anayodaiwa maiti ya Mwenyezi Mungu au ya wanadamu. Na baada ya wasia ambazo maiti aliusia ziwe baada ya kifo chake. Basi chenye kusalia baada ya hayo ndiyo mali ya kurithiwa ambayo wanaistahiki warithi. Na aliitanguliza wasia pamoja na kwamba huwa baada deni kwa sababu kulitunza jambo lake, kwa sababu ni vigumu kwa warithi kulitoa. Vinginevyo, madeni yanatangulizwa mbele yake, na yanakuwa katika rasilimali. Na ama wasia, hiyo inaruhusiwa katika theluthi moja au chini yake kwa asiyekuwa jamaa ambaye si mrithi. Na ama asiyekuwa huyo, basi hautekelezwi isipokuwa kwa idhini ya warithi. Yeye Mtukufu alisema, "Baba zenu na watoto wenu, nyinyi hamjui ni nani kati yao aliye karibu zaidi kwenu kwa manufaa." Na ikiwa makadirio ya urithi yangerudishwa kwa akili zenu na chaguo lenu, basi hilo lingelileta madhara ambayo Mwenyezi Mungu tu ndiye anayeyajua zaidi. Kwa sababu ya pungufu wa akili na ukosefu wa kujua kwake kile kinachofaa kilicho bora zaidi katika kila wakati na mahali. Kwa hivyo, hawajui ni kati ya watoto au wazazi wawili ndiye mwenye manufaa zaidi kwao, na wa karibu zaidi katika kufikia malengo yao ya kidini na ya kidunia. "Hiyo ni Sheria iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima." Yani, yalifaradhishwa na Mwenyezi Mungu, ambaye alizunguka kila kitu kwa elimu, na akadhibiti yale aliyofanya kuwa sheria, na akakadiria yale aliyokadiria kwa njia bora zaidi ya kukadiria. Akili haziwezi kupendekeza mfano wa hukumu zake nzuri, zenye kuafikiana na kila wakati, mahali na hali.