Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Surah 4

An-Nisaa

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 105

إِنَّآ أَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ بِٱلْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ ٱلنَّاسِ بِمَآ أَرَىٰكَ ٱللَّهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَآئِنِينَ خَصِيمًا 105

{105} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba aliteremsha juu ya mja wake na Mtume wake Kitabu hiki kwa haki. Yani kilihifadhiwa katika kuteremshwa kwake kutokana na mashetani kukiingiza baadhi batili yao. Bali kiliteremka kwa haki na pia kinajumuisha haki. Basi habari zake ni za kweli na maamrisho yake na makatazo yake ni ya uadilifu. “Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa ukweli na uadilifu.” Na akajulisha kuwa alikiteremsha ili kihukumu baina ya watu. Na katika Aya nyingine, “Nasi tumekuteremshia wewe ukumbusho huu ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao.” Na inawezekana kwamba Aya hii inahusu kuhukumu baina ya watu katika mambo yenye ugomvi na kuhitalifiana, na ile nyingine inahusu kuibainisha dini yote, asili yake na matawi yake. Na inawezekana kwamba aya zote mbili zina maana moja, kwa hivyo inakuwa kuhukumu baina ya watu hapa kunajumuisha kuhukumu baina yao kuhusiana na damu, na heshima, na mali, na haki nyinginezo, na katika imani, na katika masuala yote ya hukumu mbalimbali. Na kauli yake, “kwa kile alichokuonyesha Mwenyezi Mungu.” Yani si kwa matamanio yako, bali kwa yale aliyokufundisha Mwenyezi Mungu na akakufunulia wahyi, kama katika kauli yake Yeye Mtukufu, “Wala hatamki kwa matamanio. Hayo siyo isipokuwa ufunuo uliofunuliwa.” Na katika hili kuna ushahidi wa kuhifadhiwa kwake yeye – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – katika yale anayofikisha kutoka kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa hukumu zote na mambo mengineyo. Na kwamba ni sharti kwa hakimu kuwa na elimu na uadilifu, kwa kauli yake, “kwa kile alichokuonyesha Mwenyezi Mungu” wala hakusema, ‘Kwa kile unachoona.’ Pia alifungamanisha kuhukumu baina ya watu na kuwa na elimu ya Kitabu. Na Mwenyezi Mungu alipoamrisha kuhukumu baina ya watu kunakojumuisha uadilifu na haki, akamkataza ukandamizaji na dhuluma ambayo ni kinyume cha uadilifu. Akasema, “Wala usiwe mtetezi wa mahaini” Yani usimbishanie niaba yule ambaye unajua hiyana yake, kama vile mwenye kudai kitu asichokuwa chake, au mwenye kukanusha haki iliyo juu yake, awe anajua hilo au anaishuku tu. Basi katika hili kuna ushahidi juu ya kuharamishwa kubishana katika batili, na kumwakilisha mwenye batili katika kubishana kwa kidini na haki za kidunia. Na maana ya Aya isiyokuwa ya moja kwa moja inaashiria kuruhusiwa kuingia katika uwakilishi katika mabishano kwa yule ambaye hajulikani kuwa na dhuluma yoyote.