Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nisaa
Surah 4

An-Nisaa

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 1

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَٰحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَآءً ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ٱلَّذِى تَسَآءَلُونَ بِهِۦ وَٱلْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا 1

{1} Yeye Mtukufu aliifungua Sura hii kwa kuamrisha kumcha Yeye na kuhimiza kumwabudu Yeye, na kuamrisha kuwaunga jamaa na kuhimiza hilo. Na akabainisha sababu inayofanya na kulazimu kila moja katika hayo, na kwamba chenye kulazimu kumcha Yeye ndiye Mola wenu Mlezi, "Ambaye aliwaumba" na akawaruzuku na akawalea kwa neema zake kubwa, ambazo katika jumla yake ni kuwaumba "kutokana na nafsi moja." Na akafanya "mkewe kutoka kwayo" ili afaaane naye ndiyo apate utulivu kwake. Na ili neema itimie kwa hilo, na apate furaha kwa hilo. Na vile vile katika yale yanayoleta na kulazimu kumcha Yeye ni kuombana kwenu kupitia kwake, na kutukuza kwenu, mpaka nyinyi mnapotaka kutimiza mahitaji yenu na haja zenu, mnazifikia kwa kuomba kupitia kwa [Mwenyezi Mungu], basi anayetaka hayo kutoka kwa mwingine husema: Ninakuomba kwa Mwenyezi Mungu kwamba ufanye jambo fulani; kwa sababu ya kile anachojua kilicho ndani ya moyo wake cha kumtukuza Mwenyezi Mungu, kinachomfanya asikatae kumwitikia aliyemwomba kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, kama mlivyomtukuza kwa hayo, basi mtukuzeni kwa kumuabudu na kumcha. Na vile vile kujulisha kuwa yeye ni “mwenye kuona.” Yani anawaona waja wake katika hali za harakati zao, na utulivu wao, na siri yao, na dhahiri yao, na hali zote yeye anawaona ndani yake, jambo ambalo linamlazimu kumchunga na kumstahi zaidi kwa kushikamana na kumcha. Na katika kujulisha kwamba Yeye aliwaumba kutokana na nafsi moja, na kwamba aliwaeneza katika pande za ardhi pamoja na kurejea kwao kwenye asili moja ili wahurumiane wao kwa wao, na wafanyiane upole wao kwa wao. Na aliunganisha amri ya kumcha na amri ya kufanyia tumbo za uzazi wema, na kuwakataza kuzikata ili kuisisitiza haki hii. Na kwamba kama inavyolazimu kutimiza haki za Mwenyezi Mungu, basi vile vile inalazimu kutimiza haki za viumbe, hasa jamaa wa karibu miongoni mwao. Bali kutekeleza haki zao ni katika haki ya Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu aliiamrisha. Na tafakari jinsi alivyoifungua sura hii kwa amri ya uchamungu, na kuunga matumbo ya uzazi, na wanandoa kwa ujumla, kisha baada ya hapo akaeleza mambo haya kwa undani kabisa, kuanzia mwanzo wa surah hadi mwisho wake. Na ni kana kwamba imejengeka juu ya mambo haya yaliyotajwa, ikifafanua yale yaliyojumuishwa kwayo, na yenye kubainisha yale yenye maana zaidi ya moja. Na katika kauli yake, “na akamuumba mkewe kutoka kwayo” kuna kujulisha kuhusu kuzichunga haki za waume na wake na kuzitekeleza. Kwa sababu, wake wameumbwa kutokana na waume; kwa hivyo, kati ya waume na wake kuna nasaba ya karibu zaidi, na muungano mkubwa sana, na uhusiano madhubuti kabisa.