Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Saad
Surah 38

Saad

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 8

أَءُنزِلَ عَلَيْهِ ٱلذِّكْرُ مِنۢ بَيْنِنَا ۚ بَلْ هُمْ فِى شَكٍّ مِّن ذِكْرِى ۖ بَل لَّمَّا يَذُوقُوا۟ عَذَابِ 8

{8} "Ati yeye tu ndiye aliyeteremshiwa mawaidha peke yake katika sisi?" Yaani, ni kitu gani kilichomfanya bora zaidi yetu hata Mwenyezi Mungu akamshukishia yeye tu ukumbusho badala yetu? Hii pia ni fikira potofu ya utata, lakini uko wapi ushahidi ndani yake wa kukanusha alichosema? Je, si kweli kwamba Mitume wote walikuwa hivi? Mwenyezi Mungu alikuwa akiwaneemesha kwa ujumbe wake na anawaamuru kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu. Na kwa sababu maneno haya waliyosema hayakufailia hata kidogo kukanusha yale aliyokuja nayo Mtume, Mwenyezi Mungu Mtukufu alitueleza ni wapi yalitoka: 'Na kwamba wao "wana shaka na mawaidha yangu," hawana elimu yoyote wala ushahidi ulio wazi.' Walipoingiwa na shaka na wakairidhia na ikawajia haki iliyo wazi, lakini walikuwa wameshaazimia kuendelea na shaka yao, wakasema yale waliyoyasema ili kuipinga haki hiyo si kwa msingi wa ushahidi ulio wazi kuhusiana na jambo lao hilo, bali ilikuwa ni kwa mbinu ya kuzua uongo. Inajulikana kwamba mtu aliye na tabia hii atazungumza kwa shaka na ukaidi. Basi maneno yake hayatakubalika na wala si kuikashifu haki hata kidogo. Na kwamba yeye ndiye anayefaa kukaripiwa na kulaumiwa pindi anapoanza kuzungumza. Ndiyo maana akawatishia kwa adhabu, akasema: "Bali hawajaionja adhabu yangu." Yaani, walifanya ujasiri wa kusema haya maneno na wakaendelea kustareheshwa katika dunia hii bila ya kupatwa na adhabu yoyote ya Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa wangeliionja adhabu yake, basi hawangefanya ujasiri wa kufanya hivyo.