Faatir
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ أَنتُمُ ٱلْفُقَرَآءُ إِلَى ٱللَّهِ ۖ وَٱللَّهُ هُوَ ٱلْغَنِىُّ ٱلْحَمِيدُ 15
{15} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaongelesha watu wote, na kuwajulisha hali zao na sifa zao. Na kwamba wao ni masikini mbele ya Mwenyezi Mungu kwa namna zote: Ni wahitaji katika kuwaumba. Kwani, lau asingewaumba, wasingelikuwepo. Nao pia ni wahitaji katika kuwatayarisha na nguvu ambayo lau asingewatayarisha kwa hiyo, wasingejiandaa kwa ajili ya kazi yoyote ile. Nao pia ni wahitaji katika kuwapa kutoa chakula, riziki, neema za dhahiri na zilizofichikana. Na lau kuwa si fadhila zake, wema wake, na kuwasahilishia mambo, basi wasingeliweza kupata riziki wala neema yoyote. Nao pia ni wahitaji katika kuwazuilia adhabu, machukizo, dhiki na magumu. Kwa hivyo, kama hangewazuilia hayo na kuwaondolea dhiki na ugumu wao, machukizo na magumu yangeendelea kuwapata. Nao pia ni wahitaji katika kuwalea kwa aina mbalimbali za malezi na uendeshaji. Na ni wahitaji kwake katika kumfanya kuwa ndiye mungu wao, kumpenda kumuabudu, kumkusudia Yeye tu katika ibada. Na kama hangewawezesha kufanya hivyo, wangeangamia na nafsi zao, mioyo yao, na hali zao zingeharibika. Nao pia ni wahitaji kwake katika kuwafunza yale wasiyoyajua, na kutenda yale ambayo yanawafanya kuwa vizuri. Na kama asingewaliwafunza, basi hawangejifunza. Na kama hangewawezesha, hawangekuwa vizuri. Kwa hivyo, wao ni wahitaji kwake kwa dhati zao kwa kila maana ya uhitaji na kila hali ya mazingatio ya hilo, hata kama watahisi aina fulani za uhitaji au la. Lakini aliyewezeshwa miongoni mwao ni yule anayeendelea kuhusu uhitaji wake katika kila hali miongoni mwa hali zake za kidini yake na dunia, na kumuomba kwa unyenyekevu na kumuomba asimwachie nafsi yale kwa kiasi cha kupepesa jicho, na amsaidie katika mambo yake yote, na aihisi maana hii kila wakati. Mtu kama huyu anastahiki zaidi kusaidiwa kikamilifu kutoka kwa Mola wake Mlezi na Mungu wake, ambaye ni mwingi wa rehema zaidi kwake kuliko mama kwa mtoto wake. "Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa." Yaani, mwenye ukwasi kamili kwa namna zote. Hahitaji kile ambacho viumbe vyake vinakihitaji, na hapungukiwi na chochote ambacho viumbe vyake vinapungukiwa, na hilo ni kwa sababu ya ukamilifu wa sifa zake, na ukweli kwamba zote ni sifa za ukamilifu na utukufu. Na katika ukwasi wake Mtukufu ni kwamba Yeye ndiye anayewatosheleza viumbe duniani na akhera. Naye ni Msifiwa katika dhati yake na majina yake. Kwa sababu majina hayo ni mazuri zaidi, na sifa zake ni za juu zaidi, na kwa sababu matendo yake ni fadhila, ihsani, uadilifu, hekima, na rehema, na katika maamrisho yake na makatazo yake. Yeye ndiye Msifiwa kwa yale yaliyomo ndani yake na kwa yale yatokayo kwake, na ni Msifiwa katika ukwasi wake, Mkwasi katika sifa zake.