Al-Ankaboot
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِٱلْعَذَابِ ۚ وَلَوْلَآ أَجَلٌ مُّسَمًّى لَّجَآءَهُمُ ٱلْعَذَابُ وَلَيَأْتِيَنَّهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ 53
{53} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha juu ya ujinga wa wale wanaomkadhibisha Mtume na yale aliyokuja nayo, na kwamba wanasema kwa njia ya kutaka adhabu ishuke haraka na kwa njia ya kukadhibisha; "Ni lini ahadi hii, ikiwa nyinyi ni wakweli?" Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema, "Na lau kuwa hapana wakati maalumu uliowekwa;" na ambao bado haujafika, "basi adhabu ingeliwajia" kwa sababu ya kuona kwao kwamba hatuna uwezo wa hilo na kwa sababu ya kukakadhibisha kwao haki. Na kama tungewaadhibu kwa ujinga wao, basi maneno yao hayo yangewasababishia mateso na adhabu ya haraka zaidi, lakini pamoja na hayo; wasione kwamba kuteremka kwake kuko mbali sana, kwani itawajia tu "kwa ghafla ilhali wao hawana habari." Kisha ilitokea, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyowaambia, walipokuja huko Badr kwa kiburi na kujifahirisha, wakidhani kwamba wana uwezo juu ya makusudi yao. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaangamiza na wakubwa wao wakauawa, na hayo yakawa yamewapata wengi wa wakuu wao, na hakuna nyumba iliyobakia miongoni mwao isipokuwa msiba huo uliikumba. Basi ikawa imewajia kutokea ambapo hawakutarajia, na ikawafika ilhali hawaihisi.