Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Ash-Shu'araa
Surah 26

Ash-Shu'araa

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 227

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَذَكَرُوا۟ ٱللَّهَ كَثِيرًا وَٱنتَصَرُوا۟ مِنۢ بَعْدِ مَا ظُلِمُوا۟ ۗ وَسَيَعْلَمُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ أَىَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ 227

{227} Na alipowaelezea washairi kwa yale aliyowaelezea kwayo, akawaondoa katika hilo wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wakafanya matendo mema, na wakazidisha kumdhukuru Mwenyezi Mungu na kuwashinda maadui zake, washirikina baada ya kudhulumiwa nao, kwa hivyo yakawa mashairi yao katika matendo mema na athari za imani yao; kwa sababu yalijumuisha kuwasifu watu wa imani na kuwashinda watu wa ushirikina, ukafiri, na kutetea dini ya Mwenyezi Mungu, na kufafanua elimu zenye manufaa, na kuhimiza juu ya tabia njema. Alisema, "Isipokuwa wale walioamini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapodhulumiwa. Na wanaodhulumu watakuja jua mgeuko gani watakaogeuka," katika mahali pa kusimama na kuhesabiwa ambapo hayaachwi madogo wala makubwa, isipokuwa yatahesabiwa, wala haki, isipokuwa itatimizwa kikamilifu. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.