An-Noor
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
وَقُل لِّلْمُؤْمِنَـٰتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَـٰرِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ ءَابَآئِهِنَّ أَوْ ءَابَآءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَآئِهِنَّ أَوْ أَبْنَآءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَٰنِهِنَّ أَوْ بَنِىٓ إِخْوَٰنِهِنَّ أَوْ بَنِىٓ أَخَوَٰتِهِنَّ أَوْ نِسَآئِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُهُنَّ أَوِ ٱلتَّـٰبِعِينَ غَيْرِ أُو۟لِى ٱلْإِرْبَةِ مِنَ ٱلرِّجَالِ أَوِ ٱلطِّفْلِ ٱلَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا۟ عَلَىٰ عَوْرَٰتِ ٱلنِّسَآءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ ۚ وَتُوبُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَ ٱلْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ 31
{31} Alipowaamuru Mola Waumini wanaume wainamishe macho yao na wazilinde tupu zao; akawaamrisha Waumini wanawake kufanya hivyo, na akasema, ''Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao'' wasitazame uchi na wanaume kwa matamanio na kwa namna ile ya mtazamo uliokatazwa. ''Na wazilinde tupu zao.'' Wasipate kumuingilia, au kumgusa, au kumtazama kwa haramu, ''Wala wasionyeshe uzuri wao;'' kama mavazi mazuri, na mapambo, na mwili wote kwa ujumla ni katika mapambo. Na kwa vile vazi linaloonekana ni la lazima kwake yeye, alisema, “isipokuwa unaodhihirika.” Yaani, vazi linaloonekana ambalo ni desturi kuvaa ikiwa hakuna kitu ndani yake kitakacholeta majaribu ndani yake. “Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao.” Na hii ni ili kukamilisha sitara. Na hilo linaashiria kwamba, mapambo ambayo ni haramu kuyadhihirisha ni pamoja na mwili mzima, kama tulivyotaja. Kisha akakariri makatazo ya kuonyesha mapambo yao. Na kuwavua na kuwatoa katika hilo, kauli yake, ''ila kwa waume zao.'' ''Au baba zao, au baba wa waume zao,'' ni pamoja na baba mwenyewe na babu, kwenda juu, ''au watoto wao, au watoto wa waume zao." Na inajumuisha wana, au wana wa waume, hata wawe chini kiasi gani, ''au kaka zao, au wana wa kaka zao.'' Ndugu mliotoka kwa baba na mama mmoja, au ndugu wa baba mmoja au mama mmoja. ''Au wana wa dada zao, au wanawake wenzao.'' Yaani, inafaa kwa wanawake kutazamana kwa ujumla, na inawezekana kuwa nyongeza hiyo inahitaji jinsia. Yaani, wanawake wa Kiislamu ambao ni wa jinsi yenu. Na ndani yake kuna dalili kwa aliyesema: Hairuhusiwi kwa mwanamke wa Kiislamu kuangalilwa na mwanamke asiyekuwa Muislamu chini ya utawala wa Kiislamu. ''Au iliyowamiliki mikono yao ya kuume.'' Inaruhusiwa kwa anayemilikiwa ikiwa mali yote ni ya mwanamke, inafaa kwake kumwangalia bibi yake maadamu anamiliki yote. Ikiwa utaondoka umiliki au sehemu ya umiliki huo, basi haifai kuangalia, ''Au wafwasi wanaume wasio na matamanio.'' Yaani, [au] wale wanaowafuata na wakashikamana na nyinyi miongoni mwa wanaume ambao hawana hisia katika matamanio haya. Kama mpumbavu asiyejua kilichoko, na kama mtu asiyekuwa na hisia za kutamani wanawake, ambaye hakujabakia kwake yeye hisia za matamanio katika sehemu zake za siri au moyoni mwake. Hakika huyu hakatazwi kuangalia kwake, ''au watoto ambao hawajajua mambo yaliyohusu uke.'' Yaani, watoto ambao hawajabaleghe; Inajuzu kwao kuwatazama wanawake wasiokuwa Mahram. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akahalalisha hili kwa kusema, ''Hawajajua mambo yaliyohusu uke.'' Yaani, hawakuwa na ujuzi wa hilo, na matamanio yalikuwa bado hayajapatikana ndani yao. Hii inaashiria kwamba mwenye utambuzi mwanamke anafaa ajisitiri kwake, kwa sababu inadhihirika kwake uchi wa mwanamke. '' Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha.'' Yaani, wasiipige ardhi kwa miguu yao ili mapambo waliyoyavaa, kama vifundo vya miguu na vitu vingine, yakajulikana mapambo yake kwa sababu hiyo, na ikawa ni njia ya kuwatia majaribuni. Na huchukuliwa kutokana na mambo haya na yanayofanana na hayo msingi wa kanuni wa kuzuia njia, na kwamba ikiwa jambo linafaa lakini linapelekea katika jambo lililoharamishwa au kuna hofu ya kutokea kwake; basi atakatazwa na kuzuiwa kufanya jambo hilo. Kupiga mguu ardhini asili yake ni mubaha lakini ilipokuwa ni njia ya kujulikana mapambo, ikakatazwa na kuzuiwa. Mwenyezi Mungu alipoamrisha amri hizi nzuri, na akausiya kwa usiya uliopendekezwa ulio mwema, na ilikuwa ni jambo lisiloepukika kwamba kutakuwa na upungufu na uzembe wa muumini kufanya hivyo; Mwenyezi Mungu Mtukufu aliamrisha kwa kutubia. Akasema, ''Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini.'' [Kwa sababu Muumini humwita imani yake kwenye toba]. Kisha akafungamanisha juu ya hilo, mafanikio, na akasema, “ili mpate kufanikiwa.” Hakuna njia ya kufaulu isipokuwa kwa toba, ambayo ni kurudi kutoka katika yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu, kwa nje na ndani, kwenda kwenye yale anayoyapenda, kwa nje na ndani, yaani yaliyo wazi na yaliyofichika. Na hii inaonyesha kwamba kila Muumini anahitajika kutubia, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewahutubia waumini wote. Na ndani yake kuna kuhimiza juu ya kuitakasa toba katika kauli yake, "Na tubuni kwa Mwenyezi Mungu." Yaani, siyo kwa makusudio yasiyokuwa kwa ajili yake Mwenyezi Mungu kutokana na kusalimika na maafa ya dunia au kujionyesha kwa kutaka sifa au kusikika, na mfano wa hili katika makusudio maovu.