An-Noor
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّبِعُوا۟ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۚ وَمَن يَتَّبِعْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيْطَـٰنِ فَإِنَّهُۥ يَأْمُرُ بِٱلْفَحْشَآءِ وَٱلْمُنكَرِ ۚ وَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُۥ مَا زَكَىٰ مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ أَبَدًا وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يُزَكِّى مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ 21
{21} Na alipokataza dhambi hili mahususi; alikataza madhambi yote kwa ujumla. Akasema, “Enyi mlio amini! Msizifuate nyayo za Shetani.” Yaani, njia zake na wasiwasi wake. Hatua za Shetani zinahusisha dhambi zote zinazohusiana na moyo, ulimi, na mwili. Miongoni mwa hekima Yake Mwenyezi aliyetukuka, ni kwamba alibainisha hukumu. Nayo ni kukataza kufuata nyayo za Shetani. Na hekima ni kubainisha yale yaliyomo katika makatazo hayo kutokana na shari na ouvu unaolazimu na kuhitajika kuachwa kwake. Akasema, “Na atakayefuata nyayo za Shetani basi yeye,” yaani, Shetani, "Huamrisha uchafu.” Yaani, yale yanayoonekana na akili na sheria kuwa ni uchafu na uovu katika madhambi makubwa, pamoja na kuwa baadhi ya nafsi zimeegemea kuelekea huko. "Na maovu." Nayo ni yale ambayo akili huyakanusha wala haziyatambui. Na maasia ni hatua za shetani, haziondoki katika hilo. Basi Mwenyezi Mungu akawakataza juu ya hilo waja wake kuwa ni baraka na neema kutoka kwake kwamba wamshukuru na kumkumbuka. Kwa sababu huku ni kuwalinda wasije wakachafuliwa na uchafu, maovu na ubaya. Na katika wema wake kwao ni kwamba amewakataza, kama vile alivyowakataza kula sumu ya kufisha na nyinginezo. "Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake juu yenu, asingelitakasika miongoni mwenu kabisa hata mmoja." Yaani, kila kilichotakasika na kufuata nyayo za Shetani. Kwa sababu Shetani na askari wake huenda mbio katika kulingania na kuuboresha hilo, na nafsi huelekea kwenye uovu na kuuamrisha, na upungufu unamtawala mja kutoka pande zote, na imani haina nguvu. Na lau itatengwa na kuachwa peke yake na hizi sababu; Basi hakuna atakayetakasika kwa kusafishwa madhambi na matendo mabaya na maendeleo ya kustawi kwa kutenda mema. Hakika kutakasika hufungamana na usafi na maendeleo na kustawi, lakini neema na rehema zake zinawataka ajitakase miongoni mwenu yule mwenye kujitakasa. Na mojawapo ya dua za Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – ilikuwa ni: Ewe Mola! Ipe nafsi yangu uchamungu, na itakase, wewe ni mbora wa wanaoitakasa, wewe ndiye msimamizi wake na mlinzi wake). Ndiyo maana akasema, "Lakini Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye." Yule anayemjua kuhitaji kujitakasa basi atatakasika. Na ndiyo maana akasema, "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua."