Al-Baqara
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
وَإِذْ أَخَذْنَا مِيثَـٰقَ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ لَا تَعْبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ وَبِٱلْوَٰلِدَيْنِ إِحْسَانًا وَذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَقُولُوا۟ لِلنَّاسِ حُسْنًا وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ ثُمَّ تَوَلَّيْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا مِّنكُمْ وَأَنتُم مُّعْرِضُونَ 83
(83) Sheria hizi ni miongoni mwa misingi ya dini ambayo Mwenyezi Mungu aliiamrisha katika kila sheria kwa sababu zinajumuisha masilahi ya jumla katika kila zama na mahali. Basi hayaingiwi na ufutaji wowote kama asili ya dini. Ndio maana, Mwenyezi Mungu alituamrisha kwayo katika kauli yake "Na muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote," hadi mwisho wa aya. Basi kauli yake "Na tulipofunga agano na Wana wa Israili" haya ni kutokana na ugumu wao, na kwamba kila amri waliyoamrishwa waliiasi, na wala hawaikubali ila kwa viapo vikali na ahadi zilizofungwa imara. "Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu." Hii ni amri ya kumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na kukataza kumshirikisha. Na huu ndio msingi wa dini, kwa hivyo matendo yote hayakubaliki ikiwa huu sio msingi wake, kwani hii ni haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake. Kisha akasema, "na muwafanyie wema wazazi" yani wafanyieni wazazi wema kikamilifu. Na hili linajumuisha kila wema wa kimaneno na kimatendo ambao ni wema kwao. Na ndani yake kuna makatazo ya kuwafanyia wazazi ubaya, au kutowafanyia wema na kuwafanyia ubaya. Kwa sababu lililo la wajibu ni kufanya wema. Na kuamrisha kitu ni kukataza kinyume chake. Nao wema una vinyume viwili: kufanya ubaya, nalo ni kosa kubwa zaidi. Na kuacha kuwafanyia wema bila ya kuwafanyia ubaya. Na hili ni haramu, lakini sio lazima kutoshana na (ile aina) ya kwanza. Na vile vile inasemwa kuhusiana na kuwaunga jamaa, na mayatima, na masikini. Na maelezo ya ndani ya wema hayakomei kwa kuhesabu, bali kwa kuyafafanua kama ilivyotangulia hapo awali. Kisha akaamrisha kuwafanyia wema watu wote, akasema: "Na semeni na watu kwa wema" Na miongoni mwa maneno mema ni kuwaamrisha kufanya mema na kuwakataza maovu, na kuwafunza elimu, kuwapa salamu, na bashasha na yasiyokuwa hayo katika kila maneno mazuri. Na kwa kuwa mtu hawezi kumudu kuwapa watu wote mali zake, aliamrishwa kitu ambacho anaweza kwacho kuwafanyia wema kila kiumbe ambacho ni kusema (maneno) mema . Basi inakuwa ndani ya hayo katazo la kuwaambia watu maneno mabaya, hata makafiri. Na kwa sababu hii (Mwenyezi Mungu) Mtukufu alisema: "Wala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa." Na miongoni mwa adabu za mtu ambazo Mwenyezi Mungu amewafunza waja wake ni kwamba mtu awe safi katika maneno yake na matendo yake. Asifanye yasiyofaa, wala machafu, wala mwenye matusi, wala mgomvi. Bali awe na tabia njema, mwingi wa upole, anayeamiliana na watu wote kwa urahisi, mvumilivu kwa yale yanayompata miongoni mwa maudhi ya viumbe, kwa ajili ya kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na kutarajia malipo yake mazuri. Kisha akawaamrisha kusimamisha swala na kutoa zaka kama ilivyotangulia ya kwamba swala inajumuisha kumpwekesha anayeabudiwa, nayo zaka inajumuisha kuwafanyia wema waja. Kisha baada ya amri hii kwenu kwa haya maamrisho mazuri - ambayo ikiwa mwenye busara na akili atayatazama, ataajua kwamba katika ihsani ya Mwenyezi Mungu juu ya waja wake ni kwamba, aliwaamrisha hayo (swala na zaka) na akawapa kama neema juu yao, na akachukua ahadi juu yenu -"mkageuka" kwa kuyapa mgongo. Kwa sababu mwenye kugeuka, huenda akageuka huku ana nia ya kurejea katika yale aliyoyageuka. Lakini hawa, hawana hamu wala kurejea katika maamrisho haya. Basi tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kutosaidiwa na Mwenyezi Mungu. Na kauli yake "isipokuwa wachache tu katika nyinyi" huku ni kuondoa baadhi; ili isifikiriwe kwamba wote waligeuka. Basi akatoa habari kwamba, wachache miongoni mwao walilindwa na Mwenyezi Mungu na akawaimarisha.