Al-Baqara
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
ذَٰلِكَ ٱلْكِتَـٰبُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ 2
(2) Na kauli yake “Hiki ni Kitabu” yaani, kitabu hiki kitukufu ambacho ni kitabu kiuhakika, ambacho kinajumuisha yale ambayo vitabu vya watu wa mwanzo na wa mwisho havikujumuisha katika elimu kubwa na haki iliyo wazi. "Kisichokuwa na shaka ndani yake” basi hakina kusitasita wala shaka kwa namna yoyote ile. Na kukanusha shaka kuhusiana nacho kunalazimisha (kuwepo) kinyume chake, kwa sababu kinyume cha kusitasita na shaka ni yakini. Kwa hivyo, kitabu hiki kinajumuisha elimu ya yakini inayoondosha shaka na kusitasita. Na huu ni msingi unaomaanisha kwamba kukanusha kunakokusudiwa kusifu ni lazima kujumuishe kinyume chake, ambacho ni ukamilifu; kwa sababu ukanushaji unamaanisha kutokuwepo kwa kitu. Na kutokuwepo kwa kitu peke yake tu (bila ya kuthibitisha kinyume chake) hakuna kusifu kokote. Na pindi (kitabu hiki) kilipojumuisha yakini, na kukawa kuongoza hakupatikani ila kwa yakini; (Mwenyezi Mungu) akasema “ni uwongofu kwa wachamungu.” Nao uwongofu ndio unaoleta kuongoka kutoka kwa upotovu na mambo yasiyo ya wazi (shubuhaat), na kwa uwongofu mtu huongozwa kushika njia za manufaa. Na (Mwenyezi Mungu) alisema “uwongofu” na akafuta (yaani hakutaja) ma’amuul (yani ni uwongofu kwa nyanja gani za wachamungu). Ndiyo maana hakusema: Ni uwongofu kwa masilahi fulani, wala kwa kitu fulani; kwa sababu alikusudia kujumuisha, na kwamba ni uwongofu kwa masilahi yote ya Nyumba mbili (dunia na akhera). Kwa hivyo, kinawaongoza waja katika masuala ya kimsingi na ya tanzu, na kinabainisha haki kutoka kwa batili, na kilicho sahihi kutoka kwa kilicho dhaifu, na kinawabainishia jinsi ya kufuata njia zenye manufaa kwao katika dunia yao na akhera yao. Na alisema katika mahali pengine “ni uwongofu kwa watu” basi akawa amejumuisha (watu wote). Lakini hapa mahali na penginepo, akasema “ni uwongofu kwa wachamungu” kwa sababu (hiki kitabu) chenyewe ni uwongofu kwa watu wote. Ama wale waovu, wao hawakukinyanyulia kichwa juu (yaani hawakukijali), na hawakukubali uwongofu wa Mwenyezi Mungu, kwa hivyo hoja ikasimama juu yao kwacho, na hawakufaidika kwacho kwa sababu ya uovu wao. Na ama wachamungu ambao walifanya sababu kubwa ya kupata uwongofu ambayo ni uchamungu ambao uhakika wake ni kufanya yanayozuia ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu yake, kwa kufanya maamrisho yake na kuacha makatazo yake. Kwa hivyo, wakaongoka kwacho, na wakanufaika kunufaika kukubwa mno. Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema: “Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu, atakupeni kipambanuo.” Kwa hivyo, wachamungu ndio wanaofaidika na aya za Qur-aani na aya (ishara) za kiulimwengu. Na kwa sababu kuongoza ni kwa aina mbili: kuongoza kwa kueleza, na kuongoza kwa kuwezesha. Kwa wachamungu, wao walipata miongozo hii miwili. Na ama wasiokuwa wao, hawakupata mwongozo wa kuwezeshwa. Na mwongozo wa kueleza bila ya kuwezeshwa kuufanyia matendo (mema) sio mwongozo kamili kihakika.