Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Surah 2

Al-Baqara

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 188

وَلَا تَأْكُلُوٓا۟ أَمْوَٰلَكُم بَيْنَكُم بِٱلْبَـٰطِلِ وَتُدْلُوا۟ بِهَآ إِلَى ٱلْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا۟ فَرِيقًا مِّنْ أَمْوَٰلِ ٱلنَّاسِ بِٱلْإِثْمِ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ 188

{188} Yani msichukue mali za wengine. Na alizinasibisha nao kwa sababu Muislamu anapaswa kumpendea ndugu yake kile anachokipendea nafsi yake. Na aiheshimu mali yake kwa vile anavyoiheshimu mali yake (mwenyewe). Na kwa sababu ulaji wake wa mali ya wengine kunampa huyo mwingine ujasiri wa kula mali yake pia anapokuwa na uwezo. Na kwa vile kula kwake ni kwa aina mbili: Aina moja kwa haki, na aina nyingine kwa batili. Na kwamba iliyoharamishwa ni kuila kwa batili, Mwenyezi Mungu akazuia uharamu katika hiyo aina (ya batili). Na inaingia katika hilo kula kwa njia ya unyang'anyi, wizi, kufanya hiana katika amana au kile ulichosaidia kutumia au mfano wa hayo. Na inaingia katika hilo pia kuichukua kwa namna ya kubadilishana kubadilishana kwa haramu kama vile mapatano ya riba, na kamari zote. Hiyo yote ni katika kula mali kwa batili, kwa sababu sio kubadilishana kwa badala inaoruhusika. Na inaingia ndani yake pia kuichukua kwa sababu ya ulaghai katika kuuza, kununua, kukodisha na mfano wa hayo. Na inaingia ndani yake kuwatumia wafanyakazi na kula ujira wao. Na vile vile kuchukua ujira kwa kazi ambayo hawakuitimiza wajibu wake. Na inaingia katika hilo kuchukua ujira kwa ibada na mambo ya kujikurubisha nayo kwa Mwenyezi Mungu ambayo hayawi sahihi mpaka ukusudiwe kwazo uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na inaingia katika hilo kuchukua kutoka katika zaka, sadaka, waqfu, na wasia kwa yule ambaye hana haki humo, au kuchukua zaidi ya haki yake. Haya yote na mfano wake ni katika kula mali kwa batili, kwa hivyo hayo hayaruhusiki kwa hali yoyote ile, hata ikiwa kutakuwa na mzozo ndani yake. Na hilo likapelekwa kwa hakimu wa kisheria, na anayetaka kuila kwa dhuluma akaleta hoja yenye kushinda hoja ya yule anayestahiki, na hakimu akahukumu akampa yeye kwa hilo. Kwa sababu, hukumu ya hakimu hairuhusu kilichoharamishwa, wala haihalalishi kilichoharamishwa, bali anahukumu kulingana na anavyosikia, vinginevyo uhakika wa mambo unabaki. Kwa hivyo, hakuna raha, wala shaka, wala utulivu kwa mwenye batili katika hukumu ya hakimu. Kwa hivyo, mwenye atawasilisha hoja batili kwa hakimu, naye akahukumu kwamba yeye ndiye mshindi kwa hilo. Basi mali hiyo haiwi halali kwake, na anakuwa mwenye kula mali ya wengine kwa batili na dhambi hali ya kuwa anajua hilo. Basi adhabu yake ikawa ni kubwa zaidi, na onyo lake likawa ni kali zaidi. Na kwa kuzingatia hayo, ikiwa wakili atajua kuwa mteja wake ni batili katika madai yake, basi haitaruhusika kwake kumtetea mhaini. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Wala usiwe mtetezi wa wahaini”.