Al-Baqara
Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.
Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَعِينُوا۟ بِٱلصَّبْرِ وَٱلصَّلَوٰةِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ 153
(153) Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaamrisha Waumini kutafuta msaada katika mambo yao ya kidini na ya kidunia, “kwa subira na swala.” Subira ni kuishikilia nafsi na kuizuilia yale inayoyachukia. Nayo (subira) ni aina tatu: subira yake katika kumtii Mwenyezi Mungu mpaka uutekeleze (utiifu). Na (pili) kutokana na kumuasi Mwenyezi Mungu mpaka uache (kumuasi). Na (tatu) katika majaliwa ya Mwenyezi Mungu machungu mpaka usiwe na hasira nayo. Hivyo basi, subira ndio msaada mkubwa katika kila jambo. Na hakuna njia ya kupata mahitaji kwa asiyekuwa na subira; hususan mambo ya utiifu (ibada) ngumu yenye kuendelea. Kwani, hizo zinahitaji vikubwa mtu kuwa na subira na kumeza uchungu mgumu. Na ikiwa mwenyewe atashikamana na subira, atapata mafanikio. Na ikiwa atazuiwa na yenye kuchukiza na ugumu kutokuwa na subira na kushikamana nayo, hatapata chochote; na atanyimwa. Na vivyo hivyo maasia ambayo ni migumu mno misukumo ya nafsi na ni mikali mno mielekeo ya nafsi kwayo, nayo iko ndani ya uwezo wa mja. Basi hili haliwezi kuachwa isipokuwa kwa subira kubwa, na kuzuia misukumo na mwelekeo wa moyo wake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; na kutafuta msaada wa Mwenyezi Mungu ili amkinge kutokana nayo. Kwani, ni katika fitina kubwa. Na vivyo hivyo majaribu magumu, haswa ikiwa inaendelea. Hapo, inadhoofika nayo nguvu za kisaikolojia na za kimwili, na yanapatikana yale yanayoletwa na hayo. Ambayo ni kughadhabika, ikiwa mwenyewe hatakabiliana nazo kwa kuwa na subira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kumtegemea, kumkimbilia, na kumhitaji daima. Kwa hivyo, umeshajua kuwa mja anahitaji subira, bali analazimika kuwa nayo kwa kila hali katika hali zake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu alimuamrisha subira, na akajulisha kuwa: “Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.” Yani kwa wale ambao subira kwao ni tabia, na sifa, uwezo kwa kumsaidia, kumwezesha, na kumwongoa. Basi magumu na machukizo yakawawia rahisi kwa hayo, na kila jambo kubwa linakuwa jepesi kwao, na kila ugumu unawaondokea. Na huu ni upamoja maalumu unaolazimu mapenzi yake, msaada wake, ushindi wake, na ukaribu wake. Na haya ni malipo makubwa kwa mwenye subira. Na kama wenye subira hawangekuwa na fadhila isipokuwa kwamba waliyapata huu upamoja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi ingetosha kuwa fadhila na heshima. Na ama upamoja wa jumla, huo ni upamoja wa elimu na uwezo, kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na Yeye yu pamoja nanyi popote mlipo.” Na hii ni kwa viumbe vyote kwa ujumla. Na Mola Mtukufu aliamrisha kutafuta usaidizi katika swala, kwa sababu swala ndiyo nguzo ya dini, na nuru ya Waumini. Nayo ndicho kiunganishi baina ya mja na Mola wake Mlezi. Kwa hivyo ikiwa swala ya mja ni swala kamili, yenye kile kinachohitajika na kile ambacho ni Sunna, na moyo ambao ndio kiini chake ukawa umehudhuria ndani yake. Basi akawa mja anapoingia humo (katika swala), anahisi kuingia kwake kwa Mola wake Mlezi na kusimama kwake mbele yake kisimamo cha mja, mtumishi, mwenye adabu. Huku akikumbuka kila kitu anachosema na anachofanya. Huku amezama katika kuzungumza kwa faragha na Mola wake Mlezi na kumuomba, basi hapana shaka kwamba swala hii ni moja ya misaada mikubwa katika mambo yote. Kwa sababu, swala inakataza machafu na maovu. Na kwa sababu huku kuwepo ndani ya swala kunalazimu kwa mja moyoni mwake kuwa na sifa, na sababu inayomwita kutekeleza amri za Mola wake Mlezi. Na (pia) kuachana na makatazo yake. Hii ndiyo swala ambayo Mwenyezi Mungu alituamrisha tuombe msaada kwayo katika kila kitu.