Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Kahf
Surah 18

Al-Kahf

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 107

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّـٰتُ ٱلْفِرْدَوْسِ نُزُلًا 107

Na alipobainisha hatima ya makafiri na matendo yao, akabainisha matendo ya waumini na hatima yao, akasema:

{107} Yaani, "hakika wale walioamini" kwa mioyo yao, "na wakatenda mema" kwa viungo vyao. Na sifa hiyo inajumuisha dini yote. Itikadi zake na matendo yake, misingi yake na matawi yake ya dhahiri na ya ndani. Basi hawa pamoja na utofauti ulioko katika daraja zao za imani na matendo mema, "mashukio yao yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi." Inawezekana kwamba kilichokusudiwa na Pepo za Firdaus ni Pepo za juu zaidi, na bora zaidi kati yake, na kwamba thawabu hizi ni kwa yule aliyekamilisha imani na matendo mema, na wao ni Manabii na wa wale walio karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. Na inawezekana kwamba maana yake ni daraja zote za Pepo. Basi thawabu hizi zinajumuisha daraja zote za watu wa imani miongoni mwa wale walio karibu zaidi na Mwenyezi Mungu, na wema, na wale wa katikati, kila mmoja kulingana na hali yake, na hii [ndiyo bora zaidi] ya maana hizo mbili kwa sababu ya ujumla wake, na kwa sababu ya kuitaja Pepo kwa hali ya wingi huku imeunganishwa kwa Firdaus, na kwamba Firdaus hiyo inaitwa kwayo bustani iliyo na ukarimu au miti iliyoshikana. Na hili ni sahihi kuhusiana na Pepo. Kwa hivyo, Pepo ya Firdaus ndiyo mashukio na mahali pa ugeni kwa wenye imani na matendo mema. Na ni ugeni gani bora zaidi, mkubwa zaidi, mkuu zaidi kuliko ugeni huu wenye kila starehe ya mioyo na roho na viwiliwili? Ndani yake kuna yale ambayo nafsi hutamani na macho hufurahia, kama vile nyumba za kifahari, na bustani za kupendeza, na miti ya matunda, na ndege waimbao nyimbo nzuri nzuri, na vyakula na vinywaji vitamu, na wanawake wazuri, na watumishi, na watoto wadogo, na mito ipitayo, na mambo ya kutazamwa mazuri, na uzuri wa kihisia na usio wa kihisia, na neema ya kudumu, na ya juu zaidi. Na bora ya hayo yote na tukufu yake zaidi ni kufurahia kuwa karibu na Mwenye rehema na kupata ridhaa yake, ambayo ndiyo neema kubwa zaidi ya Peponi, na kufurahia kuona uso wake mtukufu na kusikia maneno ya Mwenye huruma kubwa, Mwingi wa kurehemu. Na ugeni huo ni kwa Mwenyezi Mungu. Ni ugeni mtukufu ulioje, na mzuri zaidi, na wa kudumu zaidi, na mkamilifu zaidi! Nao ni kubwa sana kuzungukwa na maelezo ya mmoja wa viumbe, au hata kupita ndani ya mioyo. Na ikiwa waja wangejua baadhi ya neema hizo kwa elimu ya uhakika yenye kufika katika mioyo yao, basi mioyo yao ingepeperuka kuiendea kwa sababu ya shauku kubwa, na roho zao zingekatika kwa sababu ya uchungu wa kutengana nayo, na wangeindea kwa makundi na mmoja mmoja, na wala hawangeipendelea dunia ya kuisha na starehe za kukatika na kuondoka badala yake. Na hawangeharibu nyakati zikipotea tu katika hasara, kwa kuwa kila muda mfupi katika dunia wa furaha unalingana na maelfu ya miaka mingi huko, lakini kwa kuwa kughafilika kumeenea, na imani ilidhoofika, na elimu ilipunguka, na utashi ulififia, ndiyo maana yakawa hayo yaliyokuwa. Basi hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, aliye juu, Mtukufu.