Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Hud
Surah 11

Hud

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 78

وَجَآءَهُۥ قَوْمُهُۥ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ ۚ قَالَ يَـٰقَوْمِ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِى هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ فِى ضَيْفِىٓ ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ رَّشِيدٌ 78

78. Na ndiyo maana yakatokea yale yaliyomjia moyoni, kwa hivyo wakaja "mbio mbio kwake." Yaani, wakaja mbio wakitaka kufanya uchafu na wageni wake hao. Uchafu ambao walikuwa wakiyafanya, na ndio maana akasema: "Na kabla ya haya walikuwa wakitenda mabaya;" yaani, uasherati ambao hakuna yeyote katika walimwengu aliyewatangulia kufanya hivyo. "Yeye akasema: Enyi kaumu yangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu" kuliko wageni wangu hawa- na hili ni kama Suleiman - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - alivyowaambia wanawake wawili wale kwamba atamgawanya mtoto yule ambaye walikuwa wanabishana juu yake ili ajue ukweli - na kwa sababu alijua kwamba mabinti zake hawangepatikana kwa urahisi na wala hawakuwa na haki yoyote kwao. Basi makusudio makubwa hapa yalikuwa kuzuia uchafu huu mkubwa. "Basi mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu." Yaani, ima muwe na uchamungu, na ima muniheshimu katika wageni wangu na msinifedheheshe mbele yao. "Hivyo je, hakuna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliyeongoka?" Basi akawakataza na kuwakemea, na huu ni ushahidi wa upotofu wao kutokuwa kwao na wema na uungwana.