Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Hud
Surah 11

Hud

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 120

وَكُلًّا نَّقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنۢبَآءِ ٱلرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِۦ فُؤَادَكَ ۚ وَجَآءَكَ فِى هَـٰذِهِ ٱلْحَقُّ وَمَوْعِظَةٌ وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ 120

{120} Alipotaja katika Sura hii habari za manabii yale aliyotaja, akataja hekima ya kuyataja hayo. Kwa hivyo, akasema: "Na yote tunayokusimulia katika habari za Mitume yale tunayokuimarisha kwayo moyo wako." Yaani, ili moyo wako utulie, na kuimarika, na usubiri kama wale waliokuwa na azimio kubwa miongoni mwa Mitume walivyokuwa na subira. Kwa maana, nafsi hutulia kwa kuiga wengine, na hupata nguvu ya kufanya matendo, na kutaka kushindana na wengine. Nao ukweli unaungwa mkono kwa kutaja ushahidi wake na idadi nyingi ya wale walioitekeleza. "Na katika haya" yaliyo katika sura hii "imekujia haki" ya yakini, basi hakuna shaka ndani yake kwa namna yoyote ile. Kwa hivyo, kujua haya ni katika kujua haki ambayo ndiyo sifa kuu zaidi ya nafsi. "Mawaidha na ukumbusho kwa Waumini;" yaani, ili waaidhike kwayo kwa hivyo wakakomeka na mambo yanayochukiza, na wanayakumbuka mambo yanayopendwa na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wakayafanya.