Langkau ke kandungan
Tafsir As-Saadi - Swahili · Yunus
Surah 10

Yunus

Ini ialah terjemahan Tafsir as-Saʿdī seperti yang diterbitkan oleh IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca daripada halaman-halaman laman itu. Laman itu tidak menyatakan siapa yang menterjemahkannya atau edisi cetakan mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan syarat untuk mengambil teksnya, maka hak untuk memaparkannya belum disahkan. Belum ada sesiapa yang membandingkannya dengan buku bercetak, dan tiada ulama yang menyemaknya. Setiap bahagian berada di sisi ayat-ayat yang diulasnya, iaitu teks Al-Quran daripada Tanzil, dipaparkan seperti yang ada di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh laman itu berada bersama bahagian sebelumnya, dan indeks menamakan setiap ayat sedemikian. Sabīl tidak menulis atau menterjemahkan satu pun daripadanya.

Teks daripadasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil pada 2026-10-22

Ayat 15

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَاتُنَا بَيِّنَـٰتٍ ۙ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَآءَنَا ٱئْتِ بِقُرْءَانٍ غَيْرِ هَـٰذَآ أَوْ بَدِّلْهُ ۚ قُلْ مَا يَكُونُ لِىٓ أَنْ أُبَدِّلَهُۥ مِن تِلْقَآئِ نَفْسِىٓ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ ۖ إِنِّىٓ أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّى عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ 15

{15} Yeye Mtukufu anataja ukaidi wa wale wanaomkadhibisha Mtume wake Muhammad - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - na kwamba wanaposomewa Aya za kiqur-aani zinazobainisha haki, wanazipa mgongo, na wanatafuta njia ya ukaidi, kisha wanasema kwa ujasiri na udhalimu, “Leta Qur-ani isiyokuwa hii, au ibadilishe,” basi Mwenyezi Mungu awatie mbali na rehema zake. Ni ujasiri ulioje huu wao dhidi ya Mwenyezi Mungu, na ni dhulumu kubwa iliyoje hii yao na kuzikataa Ishara zake! Ikiwa Mtume mtukufu huyu aliamrishwa na Mwenyezi Mungu awaambie, “Sema, “Haiwi kwangu.” Yaani, haifai wala haiendani nami, “niibadilishe nitakavyo mimi mwenyewe” kwani mimi ni mtume tu, na sina chochote katika jambo hilo. “Mimi sifuati isipokuwa yale ninayofunuliwa kwa Wahyi.” Yaani, sina lolote isipokuwa hilo. Kwa maana, mimi ni mja niamrishwaye. “Hakika mimi ninahofu, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu.” Hii ndiyo kauli ya kiumbe bora zaidi na adabu yake kwa maamrisho ya Mola wake Mlezi na ufunuo wake. Basi vipi wapumbavu hawa waliopotea, ambao walikusanya kati ya ujinga, upotofu, dhuluma, upinzani, ukaidi, na kumfanya Mola Mlezi walimwengu wote asiyeweza? Kwani hawahofu adhabu ya siku kuu? Kwa hivyo, Wakidai kuwa makusudio yao ni kwamba haki iwabainikie kwa ishara ambazo waliziomba, basi wao ni waongo katika hilo. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alikwisha zibainisha Ishara wanazoamini mfano wake wanadamu, naye ndiye anayezileta jinsi atakavyozifuata hekima yake ya kiungu, na rehema zake kwa waja wake.