Langsung ke konten
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Surah 9

At-Tawba

Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.

Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22

Ayat 96

يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا۟ عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا۟ عَنْهُمْ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ ٱلْقَوْمِ ٱلْفَـٰسِقِينَ 96

{96} Na kauli yake: "Wanawaapia ili muwe radhi nao." Yaani, wao pia wana lengo hili lingine kutoka kwenu, zaidi ya kugeuka tu, bali wanapenda kwamba muwe radhi nao kana kwamba hawakufanya lolote. "Lakini hata mkiwa radhi nao nyiye, basi hakika Mwenyezi Mungu hawi radhi na kaumu wavukao mipaka.” Yaani, Enyi Waumini, haiwafailii muwe radhi na yule ambaye Mwenyezi Mungu hana radhi naye. Bali ni juu yenu muwafikiane na Mola wenu Mlezi katika ridhaa yake na ghadhabu yake. Na tafakari namna alivyosema: "Basi hakika Mwenyezi Mungu hawi radhi na kaumu wavukao mipaka.” Wala hakusema: basi hakika Mwenyezi Mungu hawi radhi nao, ili hilo liashirie kwamba mlango wa toba uko wazi, na kwamba haijalishi wao au wengine wanatubu kiasi gani; kwani Mwenyezi Mungu atawakubalia toba na atakuwa radhi nao. Na ama maadamu wanavuka mipaka, basi hakika Mwenyezi Mungu hawi radhi nao, kwa sababu ya kuwepo kizuizi dhidi ya ridhaa yake, nako ni kutoka kwao katika yale aliyoyaridhia Mwenyezi Mungu miongoni mwa imani na utiifu hadi kwenye yale yanayomkasirisha miongoni mwa ushirikina, na unafiki, na maasia. Na jumla ya aliyoyataja Mwenyezi Mungu ni kuwa wanafiki wanaosalia nyuma ya kwenda katika jihadi bila ya udhuru, wakiwatolea waumini udhuru na wakadai kuwa wana udhuru wa kusalia nyuma kwao, basi wanafiki wanataka kwa hilo kwamba muwe radhi nao na mkubali udhuru wao. Ama kuwakubalia udhuru wao na kuwa radhi nao, basi hakuna upendo wala heshima kwao. Na ama kujiepusha nao, Basi Waumini wajiepushe nao kama wanavyojiepusha na mambo maovu na machafu. Na katika aya hizi, kuna uthibitisho wa kuzungumza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli Yake "Mwenyezi Mungu ametujulisha habari zenu." Na uthibitisho wa vitendo vya Mwenyezi Mungu vinavyotokea kwa kutaka na uwezo wake ni katika hili na katika kauli yake: "Mwenyezi Mungu amekwisha tujulisha habari zenu” na kuthibitisha vitendo vya hiari kwa Mwenyezi Mungu vinavyotokea kwa kutaka kwake na majaliwa yake. Na katika kauli yake hii “Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu;” alijulisha kwamba ataviona baada ya kutokea kwake. Na pia ndani yake kuna kuthibitisha kuwaridhia Mwenyezi Mungu waumini na kuwakasirikia wanafiki.