At-Tawba
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
يَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ مَا قَالُوا۟ وَلَقَدْ قَالُوا۟ كَلِمَةَ ٱلْكُفْرِ وَكَفَرُوا۟ بَعْدَ إِسْلَـٰمِهِمْ وَهَمُّوا۟ بِمَا لَمْ يَنَالُوا۟ ۚ وَمَا نَقَمُوٓا۟ إِلَّآ أَنْ أَغْنَىٰهُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ مِن فَضْلِهِۦ ۚ فَإِن يَتُوبُوا۟ يَكُ خَيْرًا لَّهُمْ ۖ وَإِن يَتَوَلَّوْا۟ يُعَذِّبْهُمُ ٱللَّهُ عَذَابًا أَلِيمًا فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ وَمَا لَهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ مِن وَلِىٍّ وَلَا نَصِيرٍ 74
{74} "Wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hawakusema; nao hakika wamekwisha sema neno la ukafiri." Yaani, wakisema maneno kama maneno ya wale waliosema miongoni mwao: “mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye mnyonge kutoka humo" na pia maneno ambayo mmoja baada ya mwingine huidhihaki kwayo Dini na Mtume. Na ikiwafikia kwamba Nabii -rehema na amani zimshukie - yamemfikia kitu katika hayo, wanamjia wakiapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba hawakusema. Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema akiwakadhibisha: "nao hakika wamekwisha sema neno la ukafiri, na wakakufuru baada ya kusilimu kwao." Basi kusilimu kwao hapo kabla hata kama dhahiri yake ni kwamba kuliwatoa katika eneo la ukafiri, maneno yao ya mwisho yanatengua Uislamu wao na yanawaingiza kwenye ukafiri. "Na wakawa na utashi mkubwa juu ya yale ambayo hawakuweza kuyafikia" na hilo ni wakati walipokuwa na utashi mkubwa wa kumuua Mtume wa Mwenyezi Mungu-rehema na Amani zimshukie-katika vita vya Tabuk; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akamsimulia habari zao kwa hivyo akamuamrisha mwenye kuwazuia na nia yao hiyo. "Na" hali ni kuwa "hawakuchukia" na wakamkashifu Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na Amani zimshukie - "isipokuwa kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwatajirisha, na Mtume wake pia kutokana na fadhila zake;" baada ya kwamba walikuwa mafukara na wahitaji. Na hili ni miongoni mwa mambo ya ajabu zaidi, kwamba wanamdharau yule ambaye aliokuwa sababu ya kuwatoa gizani kwenda katika nuru, na akawatajirisha baada ya ufukara! Basi je, haiwi haki yake juu yao isipokuwa kumtukuza, na wamuamini, na kumheshimu? [Basi mlinganiaji wa dini na mlinganiaji wa uadilifu wa kibinadamu wakakutana], kisha akawawekea mbele toba, kwa hivyo akasema: "Basi wakitubu, itakuwa heri kwao." Kwa sababu toba ndiyo msingi wa furaha ya dunia na Akhera "Na wakigeuka" wakaacha kutubia na kurejea, "Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu chungu katika dunia na Akhera." Katika dunia kwa yale yanayowasibu ya wasiwasi mkubwa, na huzuni kubwa, na huzuni juu ya nusura ya Mwenyezi Mungu kwa dini yake, na kumtia nguvu na kumtukuza kwake Nabii wake, na kushindwa kwao kupata yale wanayoyatafuta. Na katika akhera watakuwa katika adhabu ya Moto wenye mwako mkali. "Na wala hawana katika ardhi mlinzi yeyote" mwenye kusimamia mambo yao na kuwapa wanachokitafuta, "wala wa kuwanusuru;" anayeweza kuwazuilia machukizo. Na ikiwa wamekatika mbali na ulinzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi hapo ndipo kuna aina mbalimbali za uovu, na hasara, na masaibu, na kunyimwa.