Langsung ke konten
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Surah 9

At-Tawba

Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.

Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22

Ayat 42

لَوْ كَانَ عَرَضًا قَرِيبًا وَسَفَرًا قَاصِدًا لَّٱتَّبَعُوكَ وَلَـٰكِنۢ بَعُدَتْ عَلَيْهِمُ ٱلشُّقَّةُ ۚ وَسَيَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ لَوِ ٱسْتَطَعْنَا لَخَرَجْنَا مَعَكُمْ يُهْلِكُونَ أَنفُسَهُمْ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ إِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ 42

{42} "Lau ingelikuwa" kutoka kwenu ni kwa sababu ya kutafuta kitu cha karibu au manufaa ya kidunia yanayopatikana kwa urahisi au safari hii ingekuwa "safari fupi;" yaani, karibu na rahisi "basi hakika wangelikufuata" kwa sababu ya kutokuwepo taabu nyingi, "Lakini wameona ni mbali na kuna mashaka." Yaani, umbali wake ulikuwa mrefu kwao, na safari iliwawia ngumu. Ndiyo maana walipata uzito wakaacha kutoka nawe. Na hili si alama za uja, bali mja wa kweli ni yule anayemwabudu Mola wake Mlezi kwa kila hali, anayefanya ibada nyepesi na ngumu. Basi huyu ndiye mja wa Mwenyezi Mungu kwa hali zote. "Nao wataapa kwa Mwenyezi Mungu: Tungeliweza, basi bila ya shaka tungelitoka pamoja nanyi." Yaani, wataapa kwamba kubakia kwao nyuma wasitoke ni kwamba wana udhuru, na kwamba hawawezi hilo. "Wanaziangamiza nafsi zao" kwa kukaa nyuma, na kusema uwongo, na kusema yasiyo hali halisi. "Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa hakika hao ni waongo." Na lawama hii ni ya wanafiki tu, ambao walibaki nyuma ya Nabii – sala na salamu zimshukie – katika vita vya Tabuk, na wakatoa nyudhuru za uongo namna walivyotoa, basi Nabii – swala na amani ziwe juu yake – akawasamehe kwa kutoa kwa udhuru tu, bila ya kuwajaribu ili imbainikie ni nani mkweli na ni nani mwongo. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamlaumu juu ya kuharakisha huku kuwakubalia udhuru wao. Kwa hivyo akasema: