At-Tawba
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقُلْ حَسْبِىَ ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ ٱلْعَرْشِ ٱلْعَظِيمِ 129
{129} “Kwa hivyo” wakiamini, basi hiyo ni bahati yao na kuwezeshwa kwao. Na kama “wakigeuka” wakaiacha imani na matendo mema, basi endelea katika njia yako, wala usiache ulinganizi wako. Na sema: "Mwenyezi Mungu ananitosha;” yaani, Mwenyezi Mungu ananitosha katika yote yanayonisumbua. "Hakuna mungu isipokuwa Yeye tu;” yaani, hakuna mungu apasaye kuwabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. "Mimi ninamtegemea Yeye;” yaani, nimemtegemea na nina imani naye katika kuleta yenye kunufaisha na kuzuia yenye kudhuru. "Na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi.” Ambacho ndicho kiumbe kikubwa zaidi ya viumbe vyote. Na ikiwa Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi ambacho kimeenea viumbe vyote, basi kuwa kwake Mola Mlezi wa vinginevyo vyote kunastahili zaidi na kunafailia zaidi.
Imekamilika tafsiri ya Surat At-Tawba kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na neema yake. Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu mwanzo na mwisho, kwa dhahiri na ndani.