Langsung ke konten
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Surah 6

Al-An'aam

Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.

Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22

Ayat 128

وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَـٰمَعْشَرَ ٱلْجِنِّ قَدِ ٱسْتَكْثَرْتُم مِّنَ ٱلْإِنسِ ۖ وَقَالَ أَوْلِيَآؤُهُم مِّنَ ٱلْإِنسِ رَبَّنَا ٱسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَآ أَجَلَنَا ٱلَّذِىٓ أَجَّلْتَ لَنَا ۚ قَالَ ٱلنَّارُ مَثْوَىٰكُمْ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ 128

{128} Yeye Mtukufu Anasema, "Na ile Siku atakapowakusanya wote;" yaani, wazito wawili wote miongoni mwa wanadamu na majini, aliyepotea miongoni mwao na aliyempoteza mwingineye. Basi anasema akiwakemea majini waliowapoteza watu na wakawapambia uovu, na wakawaingiza katika maasia: "Enyi kundi la majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanadamu." Yaani, katika kuwapoteza na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu. Basi vipi mliyajia maharamisho yangu, mkafanya ujasiri katika kuwapinga mitume wangu, na mkasimama kumpiga vita Mwenyezi Mungu, mkifanya juhudi katika kuwazuia waja wa Mwenyezi Mungu kutoka kwenye njia yake hadi kwenye njia ya Jahiim? Basi leo hii laana yangu imewekwa juu yenu, na adhabu yangu imekuwa wajibu juu yenu, na tutawazidishia adhabu kulingana na kiasi cha ukafiri wenu na kupoteza kwenu wengine. Na hamna udhuru wowote kuuwasilisha, wala kimbilio mtakalokimbilia huko, wala mwombezi wa kuwaombea, wala dua itakayosikilizwa! Basi hapo usiulize juu ya yale yatakayowapata miongoni mwa adhabu na hizaya na mateso. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu hakutaja udhuru wowote kuwahusu. Na marafiki wasaidizi wao miongoni mwa watu, wao walitoa udhuru usiokubalika, na wakasema: "Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana baadhi yetu kwa wenzi wetu." Yaani, kila mmoja katika Majini na wanadamu alimfurahisha mwenzake na akanufaika naye. Jini alifurahia utiifu wa mwanadamu kwake, kwa kumwabudu, na kumtukuza, na kutafuta hifadhi kwake. Naye mwanadamu alifurahia kwa kupata malengo yake na kuyafikia kulingana na jini kumtumikia katika baadhi ya matamanio yake. Mwanadamu anaabudu jini, basi jini humtumikia na kumtimizia baadhi ya mahitaji ya kidunia. Yaani, tulifanya dhambi zilizotokea, na wala haziwezekani kuzitendua. "Na tumefikia muda wetu uliotuwekea;" yaani, tumefika mahali ambapo unalipia kwa matendo. Basi tufanyie sasa unavyotaka, na utuhukumu kwa utakalo, tayari hoja zetu zimekwisha katika, na hatuna udhuru wowote, na jambo ni jambo lako, na hukumu ni hukumu yako. Na ni kana kwamba katika maneno haya kuna aina fulani ya kunyenyekea upole, lakini kwa wakati usiokuwa wakati wake, na ndiyo maana akawahukumu kwa hukumu yake ya uadilifu isiyokuwa na dhulma. Akasema, "Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makazi yenu, mtadumu humo." Na kwa kuwa hukumu hii ilitokana na matakwa ya hekima yake na elimu yake, Akahitimisha Aya hii kwa kauli yake: "Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima kubwa, Mwenye kujua zaidi." Basi kama vile elimu yake ilienea kila kitu na kuvijumuisha, hekima yake isiyokuwa na kikomo imejumuisha mambo yote, na kuyaenea.