Al-An'aam
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
وَلَا تَأْكُلُوا۟ مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ ٱسْمُ ٱللَّهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُۥ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ ٱلشَّيَـٰطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰٓ أَوْلِيَآئِهِمْ لِيُجَـٰدِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ 121
{121} Na inaingia katika katazo hili vile vilivyotajiwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kama vile kile kinachochinjwa kwa ajili ya masanamu, na miungu ya washirikina. Basi hayo ni katika vile vilivyochinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, vilivyoharamishwa hasa kwa andiko la moja kwa moja. Na inaingia katika hilo vile ambavyo havikutajiwa Bismillah miongoni mwa vile vilivyochinjwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kama vile wanyama wa dhabihu na wale wanaopelekwa kama zawadi Makka, au kwa ajili ya nyama na chakula, ikiwa mchinjaji alikusudia kuacha kusema Bismillah kulingana na wengi wa wanachuoni. Na inatoka katika huu ujumla, aliyesahau kulingana na maandiko mengine yanayoonyesha kuondolewa kwa ugumu juu ya yake. Na inaingia katika Aya hii wale waliokufa bila kuchinjwa kisheria miongoni mwa wanyamafu. Hao ni miongoni mwa vile ambavyo jina la Mwenyezi Mungu halikutajwa juu yake. Na Mwenyezi Mungu aliwataja hawa hasa katika kauli yake: "Mmeharamishiwa mnyamafu," na huenda ikawa hii ndiyo sababu ya kuteremshwa kwa Aya hii. Kwa sababu ya kauli yake: "Na kwa yakini mashetani wanawaletea wahyi marafiki zao ili wabishane nanyi" bila ya elimu. Kwa maana, Washirikina walipomsikia Mwenyezi Mungu na Mtume wake wakiharamisha wanyamafu, na kuhalalisha kwake wanyama waliochinjwa kisheria, na walikuwa wakihalalisha kula nyamafu, wakasema kwa kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kubishana bila ya hoja wala ushahidi: “Je, mnakula wale mliowaua nyinyi, wala hamli wale aliowaua Mwenyezi Mungu?” Wakimaanisha kwa hilo nyamafu! Na haya ni maoni potovu ambayo hayaegemei juu ya hoja yoyote wala ushahidi, bali yanaegemea juu ya rai zao potovu, ambazo lau kuwa haki ingekuwa inaegemea juu yake, basi zingeharibika mbingu na ardhi na kila kilichomo ndani yake. Basi ameangamia mwenye kutanguliza akili hizi mbele ya sheria ya Mwenyezi Mungu na hukumu zake zinazoafikiana na masilahi ya ujumla na manufaa mahususi. Lakini hili halishangazi kutoka kwao. Kwa maana Maoni haya na yanayofanana na hayo yanatokana na wahyi wa marafiki walinzi wao miongoni mwa mashetani ambao wanataka kuwapoteza viumbe kutoka katika dini yao, na kuwaita ili wawe miongoni mwa watu wa Motoni. "Na mkiwatii" katika ushirikina wao na kuhalalisha kwao haramu na kuharamisha kwao halali, "basi nyinyi kwa hakika ni washirikina." Kwa sababu nyinyi mliwafanya wao kuwa marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, na mkaafikiana nao katika yale waliyojitenga na Waislamu kwayo. Na kwa sababu hiyo ikawa njia yenu ndiyo njia yao. Na Aya hii tukufu iliashiria kwamba yale yanayoingia katika nyoyo miongoni mwa wahyi na kuona mambo ambayo hutokea mara kwa mara miongoni mwa Masufi na mfano wao, hayaonyeshi yenyewe tu kuwa hayo ndiyo haki wala hayasadikiwi mpaka yaletwe mbele ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake. Na ikiwa vitayashuhudia kuwa yanakubaliwa, yanakubalika. Na ikiwa vitapingana nayo, basi yatakataliwa. Na kama hakuna chochote kinachojulikana kuhusiana nayo, basi itasimamwa katika hayo, kwa hivyo hayataaminiwa wala kukadhibishwa. Kwa sababu wahyi na kuonyeshwa mambo yanakuwa kutoka kwa Mwingi wa Rehema na vinatoka kwa Shetani. Basi Ni lazima kutofautisha baina yao na kupambanua. Na kwa sababu ya kutotofautisha kati ya mambo mawili haya kulitokea mchanganyiko na upotovu ambayo hawezi kuyahesabu isipokuwa Mwenyezi Mungu.