Langsung ke konten
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Maaida
Surah 5

Al-Maaida

Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.

Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22

Ayat 38

وَٱلسَّارِقُ وَٱلسَّارِقَةُ فَٱقْطَعُوٓا۟ أَيْدِيَهُمَا جَزَآءًۢ بِمَا كَسَبَا نَكَـٰلًا مِّنَ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ 38

{38} Mwizi ni yule anayechukua mali ya mwingine iliyoharamishwa kwake kwa siri bila ya ridhaa yake. Na hilo ni katika madhambi makubwa yenye kusababisha adhabu mbaya, ambayo ni kukatwa mkono wa kulia, Kama ilivyo katika kisomo cha baadhi ya Maswahaba. Na kikomo cha mkono wakati unapotajwa bila ya kubainisha ni kwenye kiwiko. Basi anapoiba, Mkono wake unakatiwa kwenye kiwiko na kurowekwa kwenye mafuta ili kuziba mishipa na damu iache kuvuja. Hata hivyo, Sunnah ilifungia ujumla wa Aya hii kwa njia kadhaa. Miongoni mwake ikiwa ni hifadhi nzuri. Kwa hivyo, ni lazima uwe wizi ulikuwa kutoka katika hifadhi nzuri. Na hifadhi nzuri ya kila mali ni ile inayoihifadhi kwa kawaida. Basi Ikiwa ataiba si kutoka katika hifadhi nzuri, hapaswi kukatwa. Na miongoni mwake ni kwamba ni lazima mali iliyoibiwa iwe nisab (kiasi maalum). Nayo ni robo ya dinari au dirhamu tatu au kilicho sawa na moja ya mbili hizo. Kwa hivyo, akiiba chochote chini ya hivyo, basi hapaswi kukatwa. Na labda hili linachukuliwa kutoka kwa neno wizi na maana yake. Kwani neno wizi linamaanisha kuchukua kitu kwa njia ambayo haiwezekani kukilinda, na hilo ni kwamba hali hiyo iwe ilikuwa imehifadhiwa vyema. Na Ikiwa haikuwa imehifadhiwa vyema, basi huo si wizi kisheria. Pia katika hekima ni kwamba ni ili usikatwe mkono kwa kitu kidogo, kisicho cha thamani kubwa. Na ilipokuwa hakuna budi kuweka kiwango, basi kiwango cha kisheria katika Sunnah kikawa kinafanya ujumla ulio katika Kitabu kuwa mahususi. Na Hekima katika kukatwa mkono katika wizi ni kwamba hilo ni kwa ajili ya kuhifadhi mali na kuzilinda, na ili kikatwe kiungo ambacho uhalifu ulitokana nacho. Na mwizi akirudia, unakatwa Mguu wake wa kushoto. Na akirudia, basi ilisemwa: unakatwa mkono wake wa kushoto, kisha mguu wake wa kulia. Na Ilisemwa kuwa azuiliwe mpaka afe. Na kauli yake, "yakiwa ni malipo ya waliyoyachuma;" yaani, kukata huko ni malipo kwa mwizi kwa alichoiba katika mali za watu. "Ndiyo adhabu ya mfano itokayo kwa Mwenyezi Mungu, yaani, kumtesa na kumhofisha mwizi na wengineo. Na ili kuwazuia wezi wakijua kuwa watakatwa wakiiba. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima," yaani, Ni mwenye Nguvu, Aliyehukumu kwa hivyo akamkata mwizi.