An-Nisaa
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَآؤُهُۥ جَهَنَّمُ خَـٰلِدًا فِيهَا وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُۥ وَأَعَدَّ لَهُۥ عَذَابًا عَظِيمًا 93
{93} Ilitangulia kwamba Mwenyezi Mungu alijulisha kwamba haitokei Muumini kumua Muumini mwingine, na kwamba kuua ni katika ukafiri wa kimatendo. Na hapa alitaja ahadi ya adhabu ya muuaji kwa kukusudia, ambayo nyoyo zinatetemeka kwayo, na nyoyo zinapasuka kwa sababu yake, na watu wenye akili wanahangaishwa nayo. Na haikuwahi kuja katika aina za madhambi makubwa kilicho kikubwa zaidi ya ahadi hii ya adhabu. Bali, wala iliyo mfano wake. Tahadhari! Nayo ni kujulisha kwamba adhabu yake ni Jahannam. Yani dhambi hii kubwa peke yake imeinuka juu zaidi kiwango cha kumlipa mwenyewe Jahannam pamoja na yale yaliyomo miongoni mwa adhabu yake kubwa, na hizaya yenye kudunisha, na ghadhabu ya Yeye afanyaye atakalo, na kupoteza kufaulu, na kuambulia patupu na kupata hasara. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu atulinde kutokana na kila sababu yenye kutuweka mbali na rehema zake. Na ahadi hii ya adhabu ina hukumu ya mfano wake miongoni mwa maandiko ya ahadi za adhabu juu ya baadhi ya dhambi kubwa na maasia ya kudumu katika Moto au kunyimwa Pepo. Na wamehitalifiana Maimamu, Mwenyezi Mungu awarehemu, katika kuifasiri, pamoja na kukubaliana kwao juu ya ubatili wa kauli ya Al-khawarij na Mu'utazila ambao wanawadumisha milele katika Moto hata wakiwa wanamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake. Lakini, lililo sahihi katika kuitafsiri ni yale aliyosema Imamu, mtafiti Shamsud-Din Ibn al-Qayyim, Mwenyezi Mungu amrehemu katika ‘Al-Madaarij.’ Alisema baada ya kutaja tafsiri za maimamu juu ya hilo na akawakosoa, akasema: Na kundi lilisema: Hakika, maandiko haya na mfano wake miongoni mwa yale yaliyotajwa ndani yake kinachohitaji adhabu, na wala hailazimu kuwepo kwa matakwa ya hukumu kuwepo kwake. Kwani, hukumu inatimia tu kwa kuwepo kwa matakwa na kutokuwepo kwa vizuizi vyake. Na makusudio ya maandiko haya ni kufahamisha kwamba hiki ni sababu ya kuadhibiwa na kinalazimu hivyo. Na tayari ushahidi ulikwisha simama juu ya kutajwa kwa vizuizi. Baadhi yake ni kupitia Ijmaa, na baadhi yake ni kwa maandiko ya waziwazi. Kwa hivyo, toba ni kizuizi kwa Ijmaa, na Tauhidi ni kizuizi kwa maandiko yaliyoripotiwa yasiyokuwa na shaka yoyote, ambayo hayana chenye kuyapinga. Na matendo mazuri makubwa yenye kufuta dhambi ni kizuizi. Na misiba mikubwa yenye kufuta dhambi ni kizuizi. Na kutekelezewa hukumu maalum za adhabu ya kisheria katika dunia ni kizuizi kulungana na maandiko. Na hakuna njia ya kutotumia maandiko haya. Kwa maana, ni lazima kutekeleza maandiko kutoka pande zote mbili. Na ndiyo maana kunakuwa na kulinganisha kati ya mazuri na mabaya ili kubaini chenye kulazimu adhabu au chenye kuizuia na kwa kufanyia kazi kile kinachozidi kingine uzito. Walisema: Na haya ndiyo unajengeka msingi wa masilahi ya Nyumba mbili hizi na madhara yake, na juu ya haya ndiyo unajengeka msingi wa hukumu za kisheria na hukumu za majaaliwa. Na haya ndiyo matakwa ya hekima inayotumika katika vilivyopo, na kwayo kuna uhusiano kati ya sababu na athari zake katika kuumba na amri. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekiwekea kila kinyume kinyume chake kinachokizuia na kukipinga, na inakuwa hukumu ni ya kingi chake. Basi nguvu inalazimu kuwepo afya na kuwa salama. Na kuharibika kwa vicheshi na kupita kwake mipaka ni kizuizi kwa utenda kazi wa kimaumbile, na kitendo cha nguvu, na hukumu inakuwa ya kile chenye nguvu zaidi kati yake. Na vile vile nguvu za dawa na magonjwa. Na mja ndani yake kuna mambo ambayo yana mwelekeo wa kuwa na afya na mambo mengine ambayo yana mwelekeo wa kuwa magonjwa. Na kila moja yake linajaribu kuzuia lingine kuwa na athari kamili na linajaribu kulipinga. Basi ikiwa moja litakuwa na nguvu dhidi ya lingine na likalishinda, basi hilo ndilo litakuwa na athari kubwa zaidi. Na kuanzia hapa inajulikana kuwa viumbe vimegawanyika katika wale watakaoingia Peponi na wala hawataingia Motoni, na kinyume chake. Na yule ambaye ataingia Motoni kisha akatoka humo, na kunakuwa kukaa kwake humo kulingana na yale yaliyo ndani yake yanayolazimu kukaa humo, na yataamua kutoka kwake haraka wepesi au polepole. Na mwenye ufahamu uliotiwa nuru, ataona kila kitu ambacho Mwenyezi Mungu ametujulisha katika Kitabu chake miongoni mwa mambo ya akhera na maelezo yake ya kina; kiasi kwamba anayashuhudia kwa kutazama kwa macho yake mwenyewe. Na anajua kwamba hili ndilo hitaji la Uungu wake Yeye Mtakatifu, Mtukufu, na Umola wake, na nguvu zake, na hekima yake. Na kwamba haiwezekani kwake kufanya kinyume cha hayo, na kunasibisha hilo kwake ni kunasibisha yasiyomfailia. Na kuyanasibisha hayo kwake ni kuyanasibisha yasiyomfailia, basi inakuwa kunasibisha hayo kwa ufahamu wake ni kama kulinasibisha jua na nyota kwa macho yake. Na hii ndiyo yakini ya imani. Nayo ndiyo inayounguza maovu kama vile moto unavyounguza kuni. Na mtu mwenye kiwango hiki cha imani haiwezekani kwake kuendelea kufanya mabaya, hata yakitoka kutoka kwake na yakawa mengi, nuru ya imani iliyo pamoja naye inamwamuru kufanya toba upya kila wakati kwa kumrudia Mwenyezi Mungu kwa idadi ya pumzi yake. Na hili ni katika ya viumbe vinavyopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu. Maneno yake yameisha. Mwenyezi Mungu aitakase roho yake na amlipe malipo mema kwa niaba ya Uislamu na Waislamu.