An-Nisaa
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
أَيْنَمَا تَكُونُوا۟ يُدْرِككُّمُ ٱلْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِى بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ ۗ وَإِن تُصِبْهُمْ حَسَنَةٌ يَقُولُوا۟ هَـٰذِهِۦ مِنْ عِندِ ٱللَّهِ ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ يَقُولُوا۟ هَـٰذِهِۦ مِنْ عِندِكَ ۚ قُلْ كُلٌّ مِّنْ عِندِ ٱللَّهِ ۖ فَمَالِ هَـٰٓؤُلَآءِ ٱلْقَوْمِ لَا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ حَدِيثًا 78
{78} Kisha akajulisha kuwa kutahadhari hakusaidii kitu dhidi ya majaaliwa, na kwamba mwenye kusalia nyuma hakumzuilii kusalia kwake huko kitu. Akasema, “Popote mtakapokuwa, mauti yatawafikia,” yani katika wakati wowote, na mahali popote. “Hata kama mtakuwa katika ngome zilizoimarishwa,” yani makasri yasiyoweza kushindika, na majumba yaliyoinuka. Na haya yote ni kuhimiza juu ya kufanya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Mara kwa kupeana matumaini katika fadhila zake na thawabu zake, na mara kwa kutishia juu ya adhabu ya kuiacha. Na mara kwa kuwajulisha kwamba haiwanufaishi wenye kusalia nyuma kusalia kwao huko, na mara kwa kurahisisha njia katika kufanya hivyo na kuifupisha.
Kisha akasema:
{78} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu wale wasiojua, wanaoyapa mgongo yale waliyokuja nayo Mitume, wanaowapinga, kwamba wakijiwa na mazuri, yani rutuba ya nchi, na wingi wa mali, na watoto, na afya, wanasema, “Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu.” Na kwamba yakiwapata mabaya. Yani ukame, na umaskini, na magonjwa, na kifo cha watoto na wapendwa, “Wakasema: Hili limetoka kwako wewe.” Yani kwa sababu ya yale uliyotuletea ewe Muhammad! Kwa sababu ya kufikiria kuna mkosi katika Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – kama vile mfano wao kufikiria kuna mkosi katika Mitume wa Mwenyezi Mungu. Kama Mwenyezi Mungu alivyojulisha kuhusu kaumu ya Firauni kwamba: “Likiwajia zuri, wanasema: Haya ni haki yetu. Na likiwajia baya, wanaona kwamba kuna mkosi katika Musa na wale walio pamoja naye.” Na kaumu ya Swalih walisema: "Wakasema, tunaona mkosi kwako na kwa wale walio pamoja nawe.” Na kaumu ya Yasin waliwaambia Mitume wao, “Hakika, sisi tumeona mkosi kwenu nyinyi. Kwa hivyo, ikiwa hamtaacha, basi kwa yakini tutawapiga mawe,” hadi mwisho wa Aya. Na nyoyo zao zilipofanana kwa kukufuru, yakafanana maneno yao na vitendo vyao. Na vile vile, kila mwenye kufungamanisha kutokea kwa ovu, au kutoweka kwa heri na yale waliyoyaleta Mitume au baadhi yake, basi anaingia katika lawama hii kali. Mwenyezi Mungu akasema katika kuwajibu, “Kila moja yake” yani mazuri na mabaya, mema na maovu, “ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Yani kwa hukumu yake na majaaliwa yake, na uumbaji wake. “Basi wana nini kaumu hawa,” yani ambao usemi huo wa batili ulitoka kwao, “hawakaribii kufahamu maneno?” Yani hawaelewi maneno kabisa, wala hawako karibu na kuyafahamu, au hawafahamu kwayo isipokuwa ufahamu dhaifu. Na vyovyote iwavyo, hii ni lawama kwao na kuwakemea kwa kukosa kwao kuelewa na kufahamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kutoka kwa Mtume wake. Na hilo ni kwa sababu ya kufuru yao na kupena kwao mgongo. Na katika hilo kuna kumsifu mwenye kufahamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuhimiza juu ya hilo, na juu ya sababu za kusaidia juu ya hilo miongoni kuyaelekea maneno hayo wawili, na kuyatafakari, na kuchukua njia zenye kufikisha kwayo. Na lau kuwa walifahamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi wangejua kuwa heri na maovu, na mazuri na mabaya yote ni kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na majaaliwa yake, hakuna kitu kinachoweza kutoka nje ya hayo. Na kwamba Mitume, amani iwe juu yao, hawakuwa sababu ya uovu wowote unaotokea. Si wao, wala yale waliyokuja nayo. Kwa sababu, walitumwa na masilahi ya dunia, na Akhera na Dini.