An-Nisaa
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
وَإِنَّ مِنكُمْ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنْ أَصَـٰبَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَالَ قَدْ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَىَّ إِذْ لَمْ أَكُن مَّعَهُمْ شَهِيدًا 72
{72} Kisha akajulisha kuhusu wenye Imani dhaifu, wavivu juu ya Jihadi. Akasema, “Na hakika yupo kati yenu” yani enyi Waumini, “anayejikokota sana.” Yani anaona uzito mkubwa kuhusu kufanya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kujidhoofisha, na kujilegeza, na woga. Hili ndilo sahihi. Na ilisemwa kuwa maana yake ni kwamba wao huwafanya wengine kujikokota. Yani kwa kumkatisha tamaa ya kupigana vita. Na hawa ndio wanafiki. Lakini (maana) ya kwanza ndio inayofaa zaidi kwa sababu mbili: moja yake ni kauli yake, “kati yenu”, na mazungumzo haya ni kwa Waumini. Na ya pili ni kauli yake mwishoni mwa Aya, “kama kwamba hapakuwa mapenzi baina yenu na yeye” kwa maana makafiri miongoni mwa washirikina na wanafiki, Mwenyezi Mungu alikwisha kata mapenzi baina yao na Waumini. Na pia, huu ndio ukweli. Kwani, Waumini wapo aina mbili: wakweli katika imani yao, ambao hilo liliwaletea kusadiki kukamilifu na Jihadi. Na walio dhaifu, waliingia katika Uislamu, kwa hivyo wakawa na imani dhaifu ambayo haikuwa na nguvu juu ya Jihadi. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, “Mabedui walisema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni: Tumesilimu...” hadi mwisho wa Aya hizi. Kisha akataja malengo ya hawa wanaozembea na mwisho wa malengo yao, na kwamba lengo lao kubwa ni dunia na mapambo yake. Kwa hivyo, akasema, “Na ukiwapata msiba,” yani kushindwa, na kuuawa, na maadui wakawapiku katika baadhi ya hali kwa sababu ya hekima ya Mwenyezi Mungu katika hilo, “anasema” huyo mwenye kubaki nyuma; “Hakika Mwenyezi Mungu amenineemesha kwa vile sikuwa nimehudhuria pamoja nao.” Aliona kutokana na udhaifu wa akili yake na imani yake kwamba kukaa nyuma ya Jihadi ambayo ina msiba huo ni neema. Lakini hakutambua kwamba neema ya kihakika ni kuwezeshwa juu ya utiifu huu mkubwa ambao kwao imani inaimarika, na mja anasalimika kutokana na adhabu na hasara. Na ndani yake anapata thawabu kubwa na ridhaa ya Mkarimu, Mwenye kutunuku. Na ama kukaa, basi hilo hata kama atapumzika kwa muda kidogo, basi hilo linafuatwa na taabu ndefu, na maumivu makubwa, na yanamkosa yale yanayowapata wanaopigana Jihadi.