An-Nisaa
Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.
Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22
يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لَا تَغْلُوا۟ فِى دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلْحَقَّ ۚ إِنَّمَا ٱلْمَسِيحُ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ ٱللَّهِ وَكَلِمَتُهُۥٓ أَلْقَىٰهَآ إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ ۖ فَـَٔامِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ ۖ وَلَا تَقُولُوا۟ ثَلَـٰثَةٌ ۚ ٱنتَهُوا۟ خَيْرًا لَّكُمْ ۚ إِنَّمَا ٱللَّهُ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۖ سُبْحَـٰنَهُۥٓ أَن يَكُونَ لَهُۥ وَلَدٌ ۘ لَّهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا 171
{171} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawakataza Watu wa Kitabu kupita kiasi katika Dini inayovuka. Nalo ni kupita kiwango na kiasi kinachoruhusiwa kisheria na kufikia yale ambayo hayaruhusiwi kisheria. Na hilo ni kama walivyosema Wakristo katika kupita kwao kiasi juu ya Isa, amani iwe juu yake, na kumnyanyua zaidi ya nafasi ya unabii na utume hadi kwenye nafasi ya umola ambao haufailii asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Vile vile kudunisha hadhi na kupuuza vimeharamishwa; basi kupita kiasi pia ni vivyo hivyo. Na ndiyo maana akasema, "wala msiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu ." Na maneno haya yanajumuisha mambo matatu, mambo mawili yametakazwa, nayo ni kusema uongo juu ya Mwenyezi Mungu na kusema bila ya elimu katika majina yake, na sifa zake, na vitendo vyake, na sheria yake, na mitume wake. Na la tatu limeamrishwa [kufanywa], nalo ni kusema ukweli katika mambo haya. Na kwa kuwa hii ni kanuni ya jumla kabisa, na kwamba muktadha unaomhusu Isa, amani iwe juu yake, ni andiko juu ya kusema haki kumhusu kinyume na njia ya Uyahudi na Ukristo. Akasema, "Hakika, Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Yaani, mwisho wa Masihi amani iwe juu yake, na kiwango cha juu zaidi katika daraja za ukamilifu anachoweza kufikia ni hali ya juu kabisa inayokuwa ya viumbe, ambayo ni daraja ya utume, ambayo ndiyo daraja ya juu zaidi na thawabu tukufu zaidi. Na kwamba yeye ni “neno lake tu alilomfikishia Maryam.” Yani neno ambalo Mwenyezi Mungu alizungumza kwalo, na kwalo akawa Isa, naye hakuwa ndiye hilo neno, bali alikuwa kwa hilo. Na hili ni katika mlango wa kuambatanisha kwa ajili ya kuheshimu na kutukuza, na vile vile kauli yake, "Na ni roho iliyotoka kwake." Yaani, miongoni mwa roho ambazo aliziumba na akazikamilisha kwa sifa njema na maadili kamilifu. Mwenyezi Mungu alimtuma roho wake, Jibril, amani iwe juu yake, na akapuliza katika uke wa Maryam, amani iwe juu yake. Naye akashika mimba ya Isa amani iwe juu yake kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, alipobainisha uhakika wa Isa , amani iwe juu yake, akawaamrisha Watu wa Kitabu kumwamini Yeye na Mitume wake, na akawakataza kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa ni wa tatu katika Utatu. Mmoja wao ni Isa, na wa pili ni Maryam. Basi hivi ndivyo walivyosema Wakristo, Mwenyezi Mungu aliwalaani. Kwa hivyo akawaamrisha waache, na akajulisha kwamba hilo ni heri kwao. Kwa sababu hiyo ndiyo inayobakia tu kwamba ndiyo njia ya wokovu, na isiyokuwa hiyo, hiyo ni njia ya maangamivu. Kisha akajitakasa kutokana na washirika na mwana, akasema, "Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu." Yaani, Yeye ndiye wa kipekee katika uungu, ambaye haifai ibada isipokuwa kwa ajili yake. "Subahanahu;" yaani, yuko mbali na machafu (mabaya) na ametakasika, "kuwa na mwana." Kwa sababu, "Ni vyake Yeye vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi." Kila kitu ni miliki yake, vinamhitaji Yeye. Basi haiwezekani kwamba awe na mshirika miongoni mwao au mwana. Na alipojulisha kuwa Yeye ndiye Mmiliki wa ulimwengu wa juu na wa chini, na akajulisha kuwa Yeye ndiye anayesimamia masilahi yao ya kidunia na ya kiakhera, na anayevihifadhi [na atawalipa] juu yake Yeye Mtukufu.