Langsung ke konten
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Naml
Surah 27

An-Naml

Ini adalah terjemahan Tafsir as-Saʿdī sebagaimana diterbitkan IslamHouse.com di saadi.islamenc.com, dibaca dari halaman-halaman situs itu. Situs itu tidak menyebutkan siapa yang menerjemahkannya maupun edisi cetak mana yang diikutinya, dan tidak menyatakan ketentuan untuk mengambil teksnya, sehingga hak untuk menampilkannya belum diverifikasi. Belum ada yang membandingkannya dengan buku cetak, dan belum ada ulama yang meninjaunya. Setiap bagian berdiri di samping ayat-ayat yang diulasnya, yaitu teks Al-Qur’an dari Tanzil, ditampilkan sebagaimana adanya di sana; ayat yang tidak diberi ulasan tersendiri oleh situs itu berdiri bersama bagian sebelumnya, dan indeks menyebutkan setiap ayat semacam itu. Sabīl tidak menulis atau menerjemahkan satu pun darinya.

Teks darisaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)diambil 2026-10-22

Ayat 57–58

فَأَنجَيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ إِلَّا ٱمْرَأَتَهُۥ قَدَّرْنَـٰهَا مِنَ ٱلْغَـٰبِرِينَ 57 وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلْمُنذَرِينَ 58

{57 - 58} Na ndiyo maana, Mwenyezi Mungu mtukufu akasema: "Basi tukamwokoa yeye na ahali zake, isipokuwa mkewe; tukamkadiria katika waliobaki nyuma." Na hayo ni kwamba wakati Malaika walipomjia katika umbile la wageni, na watu wake wakasikia kuwahusu, wakamjia wakiwatakia uovu, naye akawafungia nje ya mlango, na jambo hilo likamuwiya gumu mno, kisha malaika hao wakawaambia juu ya hali halisi ya uwepo wao, na kwamba walikuja kumwokoa na kumtoa miongoni mwao, na kwamba walitaka kuwaangamiza, na kwamba miadi yao itakuwa asubuhi, na wakamwamuru kwamba aondoke na familia yake usiku isipokuwa mkewe; yeye kwa hakika pia atapatwa na yale yatakayowapata (kaumu yake). Kwa hivyo, akaondoka na familia yake usiku, na wakaokoka. Nao (kaumu yake) wakafikiwa asubuhi na adhabu, na Mwenyezi Mungu akawageuzia makazi yao na akafanya juu yake kuwa chini, na akawanyeshea mvua ya changarawe za udongo mgumu uliokamatana, wa Motoni, zilizotiwa alama kwa Mola wako Mlezi. Na ndiyo maana akasema hapa, "Na tukawanyeshea mvua. Basi ni ovu mno mvua hiyo ya wale waliokwisha onywa." Yaani, mvua mbaya zaidi ni mvua yao hiyo, na adhabu mbaya zaidi ni adhabu yao hiyo, kwa sababu walionywa na wakahofishwa, lakini hawakukomeka, wala hawakuacha, kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akawafikishia adhabu yake kali.